Katibu wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwanadamizi wa Polisi (SACP) Pili Mande pamoja na timu yake aliyoambatana nayo Mei 17, 2024 amekutana na kuzungumza na askari wa kike ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kuwajengea uelewa askari hao wa Mkoa wa Kilimanjaro
SACP Mande, tayari amepita Mikoa mbalimbali nchini na kukutana na askari Polisi wa Kike ikiwa ni mkakati madhubuti wa kuwajengea uwezo katika masuala ya utendaji kazi za Jeshi la Polisi kwa kuzingatia Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu na misingi ya kisheria na taratibu nyingine za nchi kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia. Picha na Jeshi la Polisi.