Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chikanamlilo wametakiwa kutoa taarifa za ukatili wa kijinisia na uhalifu pindi wafanyiwapo na waonapo vitendo viovu wakiwa njiani, shuleni, mtaani na nyumbani ili zishughulikiwe haraka na kukomeshwa.
Kauli hiyo imetolewa Mei 09, 2024 na Polisi Kata ya Ndarambo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Johnson Bilingi wakati akiwa anawajengea uelewa wanafunzi hao kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia na uhalifu.
“Ili kuepukana na vitendo vya ukatili wa kijinsia mnatakiwa kujiepusha na tamaa za vitu vidogo vidogo kama miwa kwa sababu watoto wa Ndarambo mnapenda sana kula miwa mkiwa mnaenda na mtokapo shuleni kitendo hicho hupelekea kufanyiwa ukatili sasa basi acheni hiyo tabia ili muwe salama na mtimize ndoto za maisha yenu ya baada” alisema Mkaguzi Bilingi.