Vifaa hivyo vilivyotolewa Mei 09, 2024 na Meneja wa HJFMRI Mkoani Songwe Dr. Nassoro Yahaya kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo. Vifaa vilivyotolewa ni Viti 08 na Kabati 01 kwa ajili ya kutunzia nyaraka mbalimbali za ofisi.
Kamanda Senga amelishukuru shirika hilo kwa msaada waliotoa na amewaomba kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika harakati za kutoa elimu kwa jamii kuhusu afya bora ndio msingi wa maisha ili jamii iwe salama kwa manufaa na maendeleo ya nchi yetu.
Shirika la HJFMRI ni shirika la kimataifa linalosaidia na kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya VVU nchini kwa kutekeleza hatua mbalimbali za kuzuia maambukizi ya VVU, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za matunzo na matibabu kwa waathilika wa VVU.