Dkt,Sophia kashenge mtendaji Mkuu wa ASA akiwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji Dkt,Justin Ringo, aliyevaa shat jeupe la mikono mirefu ni Dismas Masawe mwenyekiti wa Saccos hiyona huyo mwingine ni makamu wake wa Saccos ya vijana bbt katika Shamba la mradi Chinangali Dodoma
Na Lucas Raphael,Dodoma
Wakala wa Mbegu za kilimo ASA imewaka wadau mbalimbali katika sekta binafsi wenye uwezo wa kuwekeza katika kuzalisha Mbegu wazalishe kwani bado kuna uhitaji mkubwa wa Mbegu hapa Nchini.
Kauli hiyo ilitolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo ASA Dkt. Sophia Kashenge alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Saccos ya Vijana Mradi wa Jenga kesho iliyobora BBT(Building better tomorrow) katika Shamba la Chinangali Mkoani Dodoma.
Alisema kwamba serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa ajili ya kuangiza mbegu kutoka nje ya nchini hivyo ni muhimu kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwekeza kwenye eneo hilo.
“Wakala wa Asa wanamahitaji makubwa ya mbegu kwani wanaitaji kiasi kikubwa na cha kutosha cha mbegu hivyo ni muhimu kuwashirikisha wadau ili kuzalisha mbegu bora ili kuwepo na akiba ya kutosha ili serikali kupitia wakala wasiangize mbegu kutoka nje ya nchi.”alisema Dkt Kashenge
Dkt. Sophia Kashenge alisema Wakala umejionea hali ya Shamba hilo na kumwanga sifa na ubora wa mbegu ya Alizeti iliyorolewa na ASA na kuzalishwa na Saccos hiyo.
Alisema hali ya Mbegu ni nzuri na ipo katika hatua ya kukomaa huku ikiendelea kutunzwa vizuri na kikundi hicho cha vijana waliopo kwenye mpango wa BBT.
Dkt. Sophia alisema moja ya malengo ya ASA ni kufanya kazi na sekta binafsi ili kuongeza uzalishaji wa mbegu nchini na SACCOS hiyo ya vijana wa BBT ni sekta binafsi muhimu inayohusisha vijana zaidi ya 260 wakiwemo wanawake takriban 80. Wakala umeingia nao makubaliano ya kuzalisha mbegu ya Alizeti aina ya Record hekta 300.
Aliongeza kuwa katika makundi hayo ya BBT kundi la Chinangali Dodoma linazalisha Mbegu za alizeti hekta 300 huku kundi jingine la BBT wanazalisha mbegu katika shamba la Mwele Tanga wakizalisha mbegu bora ya mahindi hekta 40.
Aidha Mwenyekiti wa Saccos hiyo Dismas Massage alisema Mbegu hiyo ya Alizeti inaendelea vizuri
Alisema Wakala wa Mbegu za kilimo ASA ni Taasisi ya Serikali hivyo kama Vijana watahakikisha wanafanya kazi vizuri ili kuendelea kuaminiwa na Serikali na jamii kwa ujumla.
Alisema katika Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 300 matarajio yao ni uvunaji Tani 100
Aliwashukuru Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Kwa kuwaamini hasa ikiwa ni mara ya kwanza kufanya kazi hiyo licha ya kuendesha kilimo hicho cha Mbegu chini ya uangalizi wa wataalam wa Kilimo kutoka ASA
Alisema matarajio ya Saccos hiyo nikufanya vizuri katika sekta ya kilimo cha Uzalishaji wa Mbegu Nchini Ili kuongeza mchango katika upatikanaji wa Mbegu bora za kilimo.