Na Mwandishi wetu – Malunde 1 blog
Wizara ya kilimo kupitia bodi ya pamba nchini imetangaza bei elekezi
ya ununuzi wa zao la pamba katika msimu wa mwaka 2024/2025 ambayo ni Sh 1,150/=
kwa kilo 1 ya pamba.
Sherehe hizo zilizoambatana na uzinduzi wa ununuzi wa zao la pamba kitaifa 2024/2025 zimefanyika leo katika Kijiji cha Ndoleleji
Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga, ambapo wanunuzi wote wa pamba
watatakiwa kununua kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali katika msimu huu.
Akitoa bei hiyo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dafroza
Ndalichako amesema wilaya ya Kishapu ni kati ya Wilaya zinazofanya vizuri
katika uzalishaji wa zao la pamba lakini bado kuna changamoto ya kuwa na pamba
chafu na kutokukata masalia ya pamba ambayo yanashusha uzalishaji na kupunguza dhamani ya zao hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya pamba Tanzania Marco Mtunga amesema
wakulima wengi Kishapu bado wanalima kilimo cha mazoea kwa kusia na
kumwaga mbegu za pamba badala ya kupanda kwa kufuata kanuni za kilimo.
Mtunga amewataka wakulima kuzingatia ubora wa pamba
wanayozalisha ili kuwa na kilimo chenye tija ikiwa ni pamoja na kuepuka kuweka
maji, mchanga na kuhakikisha wanavuna katika utaratibu mzuri ili kuepuka kuweka
uchafu jambo linalosababisha kushuka kwa dhamani ya zao hilo katika soko la nje.
Kwa uande wake balozi wa zao la pamba nchini Bwana Agrey Mwanri amemshukuru mheshimiwa Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassani pamoja na waziri wa kilimo Mheshimiwa Hussein
Mohamed Bashe kwa kutoa bilioni 1.8 kwa halmashauri ya kishapu kutokana
na jitihada zilizofanywa na wananchi huku akisisitiza matumizi bora ya pembejeo
sambamba na kuzingatia namna bora ya utunzaji wa zao hilo hata baada ya kuvuna.
Zoezi la kukata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa bei ya zao la pamba.
<<<<<<TAZAMA PICHA>>>>>
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako akikabidhi fedha kwa mkulima wa zao la pamba aliyeuza mazao yake.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu William Jijimya akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kishapu , Shija Ntelezu akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa sherehe hizo za uzinduzi.
Mbunge wa Jimbo la Kishau Boniphace Butondo akizungumza wakati wa sherehe hizo za uzinduzi.