Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Serikali Dkt. Richard Sambaiga akifafanua jambo katika kikao kati ya Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Serikali Bwa. Nicholous Zacharia.
Vickness Mayao Msajili wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Serikali akiwasilisha ripoti ya Shirika hilo katika kikao kati ya Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiandika chini yale
wanayoyasikia katika kikao kati ya Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
(PICHA NA MAELEZO)
************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Bodi ya Taifa ya Uratibu na Usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs imeitaka Baraza la mashirika hayo kushughulikia changamoto za kiuendeshaji ili kuakikisha wanazingaitia ufanishi wa hali ya juu na kuondokana na migogoro baina yao na wadau wengine.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya taifa ya Uratibu na Usajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGOs,Bw.Richard Sambaiga katika kikao na wajumbe wa kamati tendaji kilichofanyika katika ofisi za NIMR Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho,Bw.Sambaiga amesema kuwa bodi inaitaka baraza kufanya mapitio ya sheria zake na kuzifanyia mabadiliko yatakayoendana na mabadiliko yaliyofanywa mara kadhaa katika sheria inayosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s.
“Kwa kuwa Sheria ya NGOs imefanyiwa mapitio ya mara kwa mara kupitia Sheria ya marekebisho Na. 11/2005 na Sheria ya marekebisho Na.3/2019 Bodi inaelekeza Baraza kufanya mapitio ya Kanuni zake ili ziweze kuendana na hali halisi”. Amesema Bw.Sambaiga.
Aidha, Bw.Sambaiga amesema kuwa mapendekezo ya mapitio ya Kanuni hizo yawasilishwe kwa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ndani ya siku 30. Kwa mujibu wa Kifungu 28(1) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bodi imepewa jukumu la kuhakikisha Kanuni zote za Baraza zinaendana na Sera na Sheria nyingine za Nchi.
Pamoja na hayo,Bw.Sambaiga ameitaka Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ndani ya siku 14 kuwe na taarifa inayotoa mpango wa kutatua changamoto za uendeshaji kwenye sekta kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali Bw.Nicholaus Zacharia amesema kuwa watakutana na kuanza kutekeleza maelekezo ya bodi lakini pia ameiomba ofisi ya msajiri kuwapatia wanasheria watakao wasaidia kupitia sheria vizuri.
Nae Msajiri wa mashirika hayo Bi.Vickness Mayao amesema kuwa baraza hilo tayari limemaliza muda wake kisheria ambapo linapaswa kudumu kwa miaka 3 lakini kutoka na changamoto mbalimbali limeladhimika kuendelea na hivi sasa lipo mwishoni kukamilisha taratibu za uchaguzi wa baraza jipya.