Rai hiyo imetolewa Aprili 23, 2024 na Polisi Kata ya Mlangali, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Robart Kasunga baada ya kufika shuleni hapo na kutoa elimu ya usalama kwa wanafunzi hao.
Mkaguzi Kasunga amewataka wanafunzi hao kuzingatia masomo na kujiepusha na michezo ya kubahatisha (Kamali) Pool Table na kujiepusha kutembea nyakati za usiku ili kuepuka kufanyiwa vitendo vya ukatili.
“Tamaa ni mbaya inakatisha malengo yako hasa kwa wanafunzi wa kike mnatakiwa kuacha tamaa za kupenda vitu vizuri ambavyo vinapelekea mpate mimba na magonjwa na kukatisha masomo na kushindwa kufikia ndoto za maisha yenu” alisema Mkaguzi Kasunga.
Naye, Kiongozi wa Wanafunzi wa Shule hiyo Bibianna Mitendo amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali na kuwajengea uelewa juu ya madhara ya ukatili na uhalifu na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.