Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Patrobas Katambi akizungumza na wafanyakazi kutoka Mawizara, Mikoa na Idara mbalimbali za sekta ya umma na binafsi wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Mei Mosi 2024 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Na; Mwandishi Wetu – Arusha
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Patrobas Katambi amefungua rasmi michezo ya Mei Mosi na kueleza umuhimu wa michezo hiyo katika kuimarisha afya za wafanyakazi.
“Michezo ni Afya, Ajira na njia nzuri ya kujenga umoja na mahusiano mema mahali pa kazi,” amesema
Mhe. Katambi amesema hayo leo Aprili 20, 2024 wakati wa uzinduzi wa michezo ya Mei Mosi Kitaifa inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Aidha, Mhe. Katambi ameeleza kuwa, Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa michezo kwa wafanyakazi katika kuongeza ufanisi kazini na kukuza maendeleo ya taifa kwa kuwa na nguvu kazi imara.
Kwa upande mwengine, amehimiza Waajiri na Vyama vya Wafanyakazi kuweka msukumo wa wafanyakazi kushiriki katika michezo sambamba na kuruhusu michezo mahala pa kazi.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa, Bi. Rose Masamu amesema ameipongeza serikali kwa kushirikiana na TUCTA kutambua umuhimu wa wafanyakazi kushiriki katika michezo.
Kwa Mwaka 2024 Michezo ya Mei Mosi inaogozwa na Kauli Mbiu isemayo “Michezo ni Afya na Ajira, Tutunze Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu” Kazi Iendelee.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Patrobas Katambi akizungumza na wafanyakazi kutoka Mawizara, Mikoa na Idara mbalimbali za sekta ya umma na binafsi wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Mei Mosi 2024 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Michezo ya Mei Mosi 2024 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Patrobas Katambi akipokea maandamano ya timu mbalimbali kutoka Mawizara, Mikoa na Idara mbalimbali za sekta ya umma na binafsi wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Mei Mosi 2024 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Mhe. Felician Mtahengerwa akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Mei Mosi 2024 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa, Bi. Rose Masamu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Mei Mosi 2024 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.