MUONEKANO wa Masjid Al Abraar Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, na kujumuika na Wananchi wa Kijiji cha Tazari katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 19-4-2024 katika Masjid hiyo.(Picha na Ikulu)
SHEHA wa Shehia ya Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja akizungumza na kutowa shukrani za Wananchi wa Kijiji cha Tazari, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 19-4-2024, wakati wa ufunguzi wa Msikiti huo uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi na kujumuika katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.(Picha na Ikulu)
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi wa Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo 19-4-02024, katika hafla ya ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Tazari baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja uliyofanyika leo 19-4-2024.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Kijiji cha Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari, uliofanyika leo 19-4-2024.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Kijiji cha Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na Ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari uliofanyika leo 19-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Tazari katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na Ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari uliyofanyika leo 19-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi wa Masjid Abraar Tazari,baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na Ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari uliyofanyika leo 19-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wananchi na Watoto wa Kijiji cha Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja,baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na Ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari uliyofanyika leo 19-4-2024 Mkoa wa Kaskzini Unguja.(Picha na Ikulu)
………………….
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al hajj Dk. Hussein
Ali Mwinyi, amesema kazi ya Misikiti sio kufanywa ibada za sala pekee, bali ni
sehemu bora ya kutoa elimu kwa jamii na kituo kizuri cha kuwafunza vijana
mambo ya kheri.
Al hajj Dk. Mwinyi, aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa Masjid Al-Abraar – Kijiji cha
Tazari Mkoa wa Kaskazini Unguja, mara baada ya Ibada ya Sala ya Ijumaa
aliyojumuika pamoja na waumini wa Kiislam wa Kijiji hicho na maeneo jirani.
Alisema, mbali ya misitiki kutumika kwa kazi kubwa ya kufanyiwa ibada pia
inajukumu la kutatua changamoto zinazoikumba jamii wakiwemo wajane, watu
wenye uhitaji baadhi yao wanaoishi kwenye mazingira magumu, watoto yatima na
watu masikini sana kwa kupata usaidizi wa jamii ziliouzunguka msikini huo.
Alhajj Dk. Mwinyi pia aliwahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuendeleza
kukithirisha ibada wakati wote kwani Mwenyezi Mungu yupo kila siku, hivyo
aliwataka waumini hao kuziendeleza wakati kama walivyojitahidi kwenye Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani na siku za Ijumaa.
Akizungmzia kuhusu hifadhi ya kitabu kitukufu cha Quran, Al hajj Dk. Mwinyi alisema
ufunguzi wa Masjid Al-Abraar – Kijijini Tazari utakua kituo kikubwa cha kuwafunza
vijana Quran kwa njia ya takhfidh, alisema, Zanzibar imepiga hatua kubwa na
yakusifiwa kwenye eneo hilo, ambalo lilijidhihirisha wazi wakati wa Mwezi mtukufu
wa Ramadhan vijana wengi walihifadhi Quran kwa njia za Takhfidh na Tajuwiid.
Pia, Alhajj Dk. Mwinyi aliwahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuendeleza umoja,
mshikamano na upendo baina yao pamoja na kuwashukuru wafadhili waliojenga
msikiti huo.
Vilevile, aliwasihi waumini wa msikiti huo kuitunza na kuikarabati na kuipatia huduma
zote kadri itakavyohitaji ili usichakae haraka.
Mapema, akizungumza kwenye ibada hiyo, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti
Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume alisema, Masjid Al-Abraar wa Kijiji cha Tazari
Mkoa wa Kaskazini Unguja unakuwa wa msikiti wa 30 kufunguliwa na Alhajj Dk.
Mwinyi ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, pia Alhajj Dk. Mwinyi
amejumuika na wananchi na waumini wa dini ya kiislamu kwa ibada ya pamoja na
sala ya Ijuma kwenye misikiti 170 ya Unguja na Pemba sambamba na kusaidia
kutatua matatizo mengi ya misikiti hiyo.
Sheikh Khalid aliongeza kuwa, Al hajj Dk. Mwinyi ameshishiriki ijitimai zisizopungua
tano kwa maeneo tofauti pamoja na kuendelea kujumuika na waumini wa Kiislam na
wananchi wa Zanzibar kwenye sala na mabaraza ya Eid kwa nyakati tofauti za
uongozi wake.
Hivyo, aliwasihi waumini hao na wananchi kuendelea kumuungamkono Rais Dk.
Mwinyi pamoja na kuendelea kumuombea dua njema kwenye majukumu yake ya
kila siku.
Wakisoma risala na historia fupi za msikiti huo, mmoja waumini msikitini hapo,
Shheikh Mohamed Wadi alisema, ujenzi wa msikiti huo ulianza mwaka 2022 baadaya msikiti wa awali kuchakaa sana hadi walipopata mfadhili aliewajengea ambao
unatarajiwa kuwa wa ghorofa tatu.
Alisema Msikiti huo unatarajiwa kuwa kituo kikubwa cha kuhifadhia na kufundishia
Quran kwa wakaazi wote wa vijiji vya Tazari, Kidoti na jimbo lote la Nungwi, Mkoa
wa Kaskazini pamoja na kutumika kwa mahitaji mbambali ya jamii sambamba na
kuahidi kuutunza vyema.
Naye, Khatibu wa sala hiyo ya Ijumaa, Sheikh Salum Hisani alihimiza umoja
kuendeleza ukoo pamoja na jitihada za kuitunza na kuisafisha misikiti nyakati zote.