Mwenyekiti wa Taasisi ya Majlis Almaarif Islamiya Tahir Khatib Tahir akizungumza na watoto yatika katika ftarisho iliyoandaliwa na Taasisi hiyo huko Welezo Wilaya ya Magharibi “A”.
Baadhi ya watoto yatima walioshiriki katika ftarisho ilyoandaliwa na Taasisi ya Majlis Almaarif Islamiya huko Welezo Wilaya ya Magharibi “A”.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na Fauzia Mussa, Maelezo
Jamii imeshauriwa kuwa karibu na watoto wao hasa katika kipindi cha Sherehe za Skukuu ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji.
Akizungumza katika futwari maalum iliyondaliwa kwaajili ya watoto yatima huko Welezo Wilaya ya Magharibi “A” Mwenyekiti wa Taasisi ya Majlis Almaarif Islamiya Tahir Khatib Tahir amesema kufanya hivyo kutasaidia kuziba baadhi ya myanya ya vitendo hivyo kujitokeza.
Ameeleza kuwa siku chache zijazo waumini wa dini ya Kiislamu watasherehekea Skukuu ya Iddil el fitri hivyo ni vyema wazazi na walezi kuongeza ulinzi kwa watoto wao katika kipindi hicho ambacho matokeo hayo huonekana kuongezeka.
“Katika kipindi cha skukuu watu wenye tabia na dhamira tofauti hukusanyika sehemu moja, endapo tutawaachia huru watoto wetu kunaweza kuchangia Kutokea Kwa vitendo hivyo .” Alieleza
Aidha amewaomba waumini wa dini ya kiislam kuendeleza ibada na kufanya mema hata baada ya kumalizika kwa mfungo kwani ibada humkataza mtu kufanya mambo machafu na maovu.
Vile vile amewashauri wazazi na walezi wanaoishi na watoto yatima kuwasajili watoto hao katika vituo vinavyotambulika ili kuwarahisihia kupatiwa misaada pale inapotokezea.
Kwaupande wake Kiongozi wa watoto hao kutoka Mtopepo Rizki daudi Haji amewashauri wazazi na walezi kuongozana na watoto wao katika viwanja vya skukuu ili kupunguza athari za udhalilishaji.
“unaweza kutoka na watoto wako mapema tu saa kumi hata saa 12, saa mbili umerudi nyumbani na watoto wako mkiwa salama” alieleza
Aidha amewaomba wazazi hao kuwavisha nguo za stara watoto wao kwani kutembea uchi ni miongoni mwa vichocheo vya udhalilishaji.
“Unapomsitiri mtoto wako au kujistiri wewe mwenyewe basi mwenyezimungu nae pia anakustiri na mambo mbalimbali” alisema
Hatahivyo amewaomba wenye uwezo kupita mitaani kuangalia watoto hao kwani sio wote walio sajiliwa katika jumuiya maalum za mayatima, na kuzishauri jumuiya hizo kushajihisha kusajiliwa kwa watoto hao kwani wakiwa katika taasisi maalum ni rahisis kufikiwa na misaada.
Nao watoto yatima walioshiriki ftari hiyo wameishukuru Taasis ya Majlis Al- Maarif Islamiya kwa kuwakumbuka na kuungana nao katika hafla hiyo pamoja na kuwaombea kipato zaidi kutoka kwa mweneyezimungu.
Kiasi cha watoto yatima 50 kutoka Mtopepo na vijiji jirani wamefutwari pamoja na Taasisi hiyo inayojishughulisha na kuwasaidia makundi maalum yakiwemo mayatima,wajane na wenye ulemavu.