WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu uliomalizika leo Aprili 5,2024 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu uliomalizika leo Aprili 5,2024 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu uliomalizika leo Aprili 5,2024 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,(hayupo pichani) wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu uliomalizika leo Aprili 5,2024 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Elimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Dkt. Daniel Baheta, wakati wa kufunga Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu uliomalizika leo Aprili 5,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imewaelekeza walimu wa shule za msingi nchini kutowarudisha nyumbani wanafunzi ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia michango mbalimbali na badala yake waachwe waendelea na masomo.
Hayo yameelezwa leo Aprili 5,2024 Jijini hapa na Waziri mwenye dhamana ya Elimu nchini Prof.Adolf Mkenda wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathmini ya Sekta ya elimu kwa mwaka 2023/2024 .
Amesema hakuna utaratibu wa kiserikali wa kumrudisha mwanafunzi nyumbani kwa kukosa michango kwa kuwa dhana ya elimu bila ada inaelekeza mtoto asinyimwe kwenda shule kwa kukosa michango na kufafanua kuwa hakuna adhabu yoyote itakayofanya mtoto akose masomo.
Waziri Mkenda ameeleza kuwa licha ya changamoto zilizopo kwenye Sekta hiyo,Walimu wanapaswa kuheshimiwa ili kuwafanya wanafunzi kuwa bora.
“Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kuleta mageuzi kuanzia ngazi ya chini hadi vyuo vikuu.”amesema Prof.Mkenda
Aidha Prof. Mkenda ameitaka jamii kushiriki kikamilifu katika michango ya chakula shuleni ili kuendelea kuiunga mkono serikali katika dhana yake ya elimu bila malipo.
“Elimu bila malipo haina maana kuwa ni elimu bure kwa sababu wazazi mnanunua madaftari na vitu vingine vya kumuwezesha mtoto kusoma bila changamoto sasa kwa sababu serikali ilishafanya kazi kubwa ya kutoa elimu bila malipo , jamii nayo ihamasike kuchangia baadhi ya michango ikiwemo chakula na isitokee mtoto akarudishwa nyumbani eti kisa hajalipa michango yeyote,” amesema Prof. Mkenda
Kwa upande wake Kamishina wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa, ameeleza kuwa wamejadili na kuazimia kwenda kuyafanyia kazi maeneo ambayo yataleta ufanisi katika wa elimu.
Aidha amesema kuwa wataboresha vikao na mikutano ya pamoja ya tathimini katika sekta ya elimu ili kuleta matokeo chanya na kuboresha mpango wa chakula na lishe mashuleni ambapo wameazimia ikiwezekana sheria itungwe ya kuwataka wazazi wachangie masuala mazima ya elimu pale inapobidi kwani bila afya akili hakuna.
“Tupeleka Sera za mitaala ili kulahisisha wadau na walimu katika utendaji kazi,kutaka elimu ya juu kuakisi mabadiliko yote yalifanyika kuanzia elimu ya ngazi ya chini, bila kusahau kuimalisha ushirikiano kati ya wizara na wadau Mbalimbali wanaotoa elimu hapa nchini na nje ya nchi . “amesema Dkt.Mtahabwa