Klabu ya Arsenal imemfungashia virago aliyekuwa kocha wake Unai Emery.
Hiyo ni kufuatia mfululizo wa matokeo mabovu yaliyowaandama klabu hiyo ambapo katika michezo saba iliyopita waliambulia vichapo vitatu na kusuluhu mara nne.
Kiungo wa zamani wa klabu hiyo Freddie Ljungberg ameteuliwa kuwa kocha wa muda mpaka kipindi watakapopata kocha mwingine.