Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Afya ya Msingi nchini Tanzania ulioambatana na uzinduzi wa namba 115 ya kuwasiliana na watoa huduma kupitia mfumo wa M-mama ulioanza leo Machi 25,2024 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Afya ya Msingi nchini Tanzania ulioambatana na uzinduzi wa namba 115 ya kuwasiliana na watoa huduma kupitia mfumo wa M-mama ulioanza leo Machi 25,2024 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anaeshughulikia Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Mhe.Dkt. Festo Dugange ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Afya ya Msingi nchini Tanzania ulioambatana na uzinduzi wa namba 115 ya kuwasiliana na watoa huduma kupitia mfumo wa M-mama ulioanza leo Machi 25,2024 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Godwin Mollel,akizungumza wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Afya ya Msingi nchini Tanzania ulioambatana na uzinduzi wa namba 115 ya kuwasiliana na watoa huduma kupitia mfumo wa M-mama ulioanza leo Machi 25,2024 jijini Dodoma..
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, akizindua namba 115 ya kuwasiliana na watoa huduma kupitia mfumo wa M-mama unaoratibiwa katika hospitali za mikoa kupitia waratibu waliopewa mafunzo.
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Afya ya Msingi nchini Tanzania ulioambatana na uzinduzi wa namba namba 115 ya kuwasiliana na watoa huduma kupitia mfumo wa M-mama leo Machi 25,2024 jijini Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,akipongeza zawadi kutoka kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anaeshughulikia Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Mhe. Festo Dugange,iliyotolewa kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua na kuthmani mchango wake katika kuimarisha huduma za Afya ya Msingi.
Mkurugenzi wa M-Mama Tanzania Bi.Dolorosa Duncan ,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Afya ya Msingi nchini Tanzania ulioambatana na uzinduzi wa namba 115 ya kuwasiliana na watoa huduma kupitia mfumo wa M-mama ulioanza leo Machi 25,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko,ameupongeza mfumo wa usafiri wa dharura kwa wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga (M-MAMA)uliobuniwa na Watanzania .
Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Afya ya Msingi nchini Tanzania ulioambatana na uzinduzi wa namba namba 115 ya kuwasiliana na watoa huduma kupitia mfumo wa M-mama unaoratibiwa katika hospitali za mikoa kupitia waratibu waliopewa mafunzo kwa ambapo kila mkoa wanaweza kutoa huduma hizo ulioanza leo Machi 25,2024 jijini Dodoma
Amesema kuwa kila mwaka akina Mama zaidi ya milioni mbili, laki tatu na sabini wanajifungua, na kati ya hao takriban akinamama elfu arobaini na tano wanapata dharura zinazohitaji usafiri kwenda kwenye kituo kinachotoa huduma stahiki kulingana na dharura hizo.
“Kwa furaha kubwa nasimama mbele yenu siku ya leo nikifurahia kuona maono ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha mfumo wa usafiri wa dharura kwa wajawazito, waliojifungua na watoto,” amesema Dkt. Biteko.
Dkt.Biteko amesema, M-mama inaratibiwa katika hospitali za mikoa kupitia waratibu waliopewa mafunzo kwa kupiga namba 115 ambapo waratibu wa m-mama katika kila mkoa wanaweza kutoa huduma hizo.
“Napenda kuwashukuru wadau wetu wa maendeleo Vodacom Tanzania, Vodafone Foundation, USAID, Benki ya Dunia na wadau watekelezaji wa mfumo wa ‘Touch Health’ na ‘Pathfinder International’ kwa mchango wao katika kushirikiana na Serikali kuleta huduma hii inayohitajika kwa wote,” amesisitiza Dkt. Biteko.
Hata hivyo Dkt. Biteko ameagiza kuweka Mpango Mkakati wa kuhakikisha uwekezaji wa miundombinu uliofanywa na Serikali katika vituo ngazi ya Afya ya Msingi inatunzwa.
Dkt. Biteko amewataka kujadili kwa kina namna bora ya kubuni mbinu zitakazowezesha kuongeza kasi ya kuajiri wataalam wa kada mbalimbali za afya hasa zile zenye upungufu mkubwa.
“Naagiza kuainisha mikakati ya utoaji wa elimu ya afya kwa jamii ili wananchi waelimishwe kuhusu njia za kuzuia magonjwa, umuhimu wa chanjo na njia zingine za kudumisha afya bora.”amesema
Dkt. Biteko amehimiza kuwezesha watu, familia na jamii kwa ujumla kuzingatia afya bora na kuhamasisha utekelezaji wa sera na miongozo inayolenga kulinda afya ya jamii.
Pia Dkt. Biteko amesisitiza kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini ya huduma za afya ya msingi ili kuweza kufahamu maendeleo ya utekelezaji wa Afua mbalimbali za afya na kutambua maeneo ya kuboresha.
Awali Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anaeshughulikia Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Mhe. Festo Dugange amesema kuwa mkutano huo unawezesha kujadiliana masuala mbalimbali na kubadilishana uzoefu na namna ya kuboresha afya ya msingi kwa watu wote.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Godwin Mollel amewashukuru wafanyakazi wa afya nchini kwa kujitolea kuboresha huduma za afya ambapo kupitia wao idadi ya vifo vya akinamama wajawazito vimepungua kutoka 556 hadi 104 mwaka 2023.