Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto,iliyopo eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, Mhe. Elizabeth Missana,(kulia) akizungumzia kuhusu mahakama hiyo kwa majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania waliopishwa hivi karibuni.
……………………
Na Magreth Kinabo-Mahakama
Mahakama ya Watoto, iliyopo eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam imefanikiwa kumaliza mashauri 438 katika kipindi cha Januari 2019 hadi Novemba 22, mwaka huu sawa asilimia 98.
Hayo yalisema na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe. Elizabeth Missana, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Novemba, 27 mwaka huu, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Alisema yaliyofunguliwa mwaka 2018 ni 406 na mwaka 2019 Januari 2019 hadi Novemba 22, mwaka huu yalifunguliwa mashauri 390.
Alisema idadi hiyo ya kesi hizo iliongezeka imekuwa ikiongezeka katika kipindi cha mwaka huu kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda la kuwataka wanawake waliozaa watoto na kutekelezwa na wanaume waliowapa ujauzito kujitokeza hadharani ili waweze kusaidiwa.
Aliongeza kuwa idadi kubwa ya mashauri iliongezeka katika kipindi cha miezi ya tisa .10 na 11, ambapo mashauri mengi ni ya madai.
Mhe. Missana alisema mpaka sasa Mahaakama hiyo ina mashauri yaliyobaki ni 151, kati ya hayo 28 ni ya mlundikano na 12 ni yale ambayo hawana mamlaka ya kuyasikiliza, lakini mashauri 14 wana mamlaka nayo ila sababu mbili zinasubiri majibu ya vipimo vya vinasaba (DNA).
Mashauri mengine 12 yamechelewa kwa sababu mashahidi wanafika mahakamani kwa kusuasua.
‘Tumefanikiwa kumaliza mashauri haya kwa sababu tulifanya vikao na wadauwa ustawi wa jamii na kuwaomba wananchi watusaidia watusaidie kuhudhuria katika mashauri hayo,’ alisema.
Katika Mahakama hiyo, mashauri yaliyobaki mwaka 2017ni 139 na yaliyoamuliwa mwaka 2018 ni 339 na yaliyobakia mwaka 2018 ni 199. Mwaka 2019 mahakama hiyo iliingia na mashauri 199.