Na Lucas Raphael,Tabora
Mkuu mpya wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amesema kwamba amekuja tabora kwa ajili ya kusimamia haki, usalama na maendeleo ya wananchi wa mkoa wa huo.
Kauli hiyo alitoa jana alipokuwa akizungumza katika kikao cha pamoja na watumishi wa kanda mbalimbali za mkoa huo wakati kukaribishwa wake kwenye ukumbi wa mtemi Isike Mwanakiyungi
Chacha alisema kwamba moja ya vipaumbele vyake ni Haki ,usalama na maendeleo,pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi hivyo kila kiongozi kuhakikisha anasimama eneo lake la kiutawala na wasaidia wananchi kuvuka hapa tulipo.
Aidha ajitambulisha kuwa yeye ni mtu mwenye msimamo, muumini wa haki na kuahidi kwamba katika kusimamia haki na maendeleo ya mkoa wa Tabora Kwa kushirikiana na viongozi na wananchi wa halmashauri zote za mkoa huo.
Hata hivyo alifafanua kwamba kuna kesi ya mauaji ambayo aliiacha miaka miwili iliyopita alipokua mkuu wa wilaya ya Kaliua ambapo mwanaume mmoja alituhumiwa kuwaua watoto wawili wa mke wake na kuwazika ndani kisha kutokomea kusikojulikana na kuliagiza jeshi la polisi kumsaka na kumkamata mtuhumiwa huyo.
Alisisitiza kwamba vitendo vya ukali kwa wanawake na watoto hatoweza kuvifumbia macho katika kipindi ambacho hatakuwa mkoani hapa hatopenda viendelee kujitokeza na kuwaomba viongozi wa dini kuhakikisha wanakemea vitendo vyote viovu.
Awali akimkaribisha mkuu wa mkoa Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya aliahidi ushirikiano Kwa niaba ya watumishi wengine wa mkoa huo.
Alisema kwamba mkoa una watumishi waadilifu na wachapa kazi ambao watamsaidia kutimiza majukumu yake mapya kama mkuu wa mkoa.
Kwa upande wake Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora Ramadhani Kapela alishukuru kwa niaba ya wenyeviti wa halmashauri za mkoa wa Tabora na kusema ni matumaini ya wengi kwamba atautumikia mkoa wa Tabora kwa ufanisi kwakua yeye si mgeni katika mkoa huo.
Mkuu wa mkoa mpya Paul Matiko Chacha anachukua nafasi ya aliyekua mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian aliyehamishiwa mkoani Tanga katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu siku chache zilizopita.