Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa na wajumbe wa Kamati, wakiwasikiliza wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rukoma katika maabara ya somo la Kemia wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule hiyo iliyopo katika Hamshauri ya Wilaya ya Bukoba.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Rukoma wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule hiyo iliyopo katika Hamshauri ya Wilaya ya Bukoba.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua ujenzi wa wa mradi wa Shule ya Sekondari Rukoma wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo uliopo katika Hamshauri ya Wilaya ya Bukoba.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akipima urefu wa msingi katika mojAwapo ya jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa hospitali hiyo.
………………
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imeisisitiza Serikali kuhakikisha inapeleka vifaa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ili majengo yaliyojengwa yaanze kufanya kazi.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa mradi huo pamoja mradi wa Shule ya Sekondari Rukoma katika Halmashauri hiyo.
Alisema Kamati inaipongeza Halmashauri kwa kukamisha ujenzi wa Hospitali hiyo lakini inasikitishwa na baadhi ya majengo kutoanza kutumika kutokana na ukosefu wa vifaa.
“Kati ya majengo kumi na tano yaliyojengwa ni majengo tisa tu yanayotumika wakati majengo sita hayajaanza kutumika kutokana na ukosefu wa vifaa,haiwezekani toka mwaka 2022 hadi leo 2024 vifaa havijaletwa, Mheshimiwa Rais analeta fedha ila sisi ni kama tumezitupa kwa kutokuleta vifaa,” alisema.
Alisisitiza Wizara ya TAMISEMI kahakikisha inaisimamia Bohari ya Dawa (MSD) ili ipeleke vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shlingi milioni 300.
Aidha, Mheshimiwa Mabula aliagiza mashine ya kufulia iliyokwishanunuliwa ipelekwe katika jingo lake ili ianze kufanya kazi.
Pamoja na mambo mengine Kamati pia ilitaka kufanyika kwa marekebisho iliyoyaainisha ikiwemo milango na sakafu.
Kwa upande wa Shule ya Sekondari Rukoma, Kamati iliagiza kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kwa wakati pamoja na kupeleka umeme.
Kamati ya LAAC ipo katika siku ya tatu ya ziara za ukaguzi wa miradi huku kesho itakuwa katika Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera na itakagua mradi wa Hospitali ya Halmashauri ya Misenyi na Shule mpya ya Sekondari Kitobo katika katika Halmashauri hiyo.