Na Koplo Issa Mwadangala wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe.
Umoja wa Waandishi wa habari mkoa wa Songwe wamemlilia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP. Theopista Mallya ambae amapangiwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ambapo wameeleza namna kamanda huyo alivyofanya kazi kwa juhudi na kuonesha ushirikiano na waandishi hao kipindi chote alichohudumu katika mkoa huo.
Hayo yalijiri wakati wa kikao cha pamoja kati ya Polisi Mkoa wa Songwe na Umoja wa Waandishi wa habari Mkoa wa Songwe (UTPC) kilichofanyika Machi 14, 2024 katika ukumbi wa Mpende Jirani Wilayani Mbozi ambapo kimejadili utekelezaji wa maazimio 11 waliojiwekea katika kikao cha awamu ya tatu kilichofanyika Februari 15, 2024.
Katika kikao hicho SACP Mallya alitumia nafasi hiyo kuwaaga waandishi wa habari kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanywa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP. Camillus Wambura
“Nachukua fursa hii kuwaaga baada ya kupangiwa kuwa Kamanda wa mkoa wa Dodoma hivyo basi nawashukuru sana waandishi wa habari kwa ushirikiano wenu kwa kipindi chote ambacho nilikuwa mkoani hapa pia najua mtaendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vyenu vya habari kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo katika jamii” Alisema Kamanda Mallya.
Nae Mwenyekiti wa Klabu hiyo Stephano Simbeye amelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari ambapo wameahidi kudumisha ushirikiano huo kwa Kamanda anaekuja ili jamii ya wanasongwe iendelee kuwa salama.
Ikumbukwe kuwa kila mwaka hufanyika midahalo 03 kati ya Jeshi la Polisi na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa lengo la kuweka mikakati ya kuendelea ushirikiano na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa kutekeleza majukumu ya kazi baina ya Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi. ushirikiano na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa kutekeleza majukumu ya kazi baina ya Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi.