Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Lemburis Mollel akitaka ufafanuzi mbele ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akitoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Masud Kibetu akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakimsikiliza Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.
……………
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kutenga fedha za kutosha ili iweze kumalizia ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.
Ushauri huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua mradi huo pamoja mradi wa Kituo cha Afya Kinaga katika Halmashauri hiyo.
Alisema kiasi cha shilingi milioni mia saba ambacho Halmashauri hutenga kwa mwaka kwa ajili ya ujenzi hakitawezesha mradi huo kumalizika kwa haraka kwa manufaa ya wananchi.
Aidha, alilisitiza uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wapatekeleza miradi yote thamani ya fedha ionekane na kwamba Kamati itarudi tena kufanya ukaguzi.
Pamoja na ushauri huo, Kamati iliupongeza uongozi wa Halmashauri kwa kuyafanyika kazi mapungufu ya awali ambayo Kamati ilielekeza yafanyiwe marekebisho.
Kamati ya LAAC inaendelea na ziara ambapo kesho itakagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na mradi wa ujenzi wa Sekondari ya Rukoma katika Halmashauri hiyo.