Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga,akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara katika mikoa yote hapa nchini ambayo wanataka kufanya kwa lengo la tatmini ya watumiaji wa Nishati kwenye maeneo ya vijijini.
Akimwakilishi Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Meneja wa Takwimu za Kilimo na Mifugo,Bw.Titus Mwisomba,akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara katika mikoa yote nchini ambayo wanataka kufanya kwa lengo la tatmini ya watumiaji wa Nishati kwenye maeneo ya vijijini,upande wa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi (Sera na Mipango) kutoka wizara ya Nishati,Oscar Kashaigili.
Kaimu Mkurugenzi (Sera na Mipango) kutoka wizara ya Nishati,Oscar Kashaigili,akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara katika mikoa yote nchini ya kufanya tatmini ya watumiaji wa Nishati kwenye maeneo ya vijijini Kulia ni Meneja wa Takwimu za Kilimo na Mifugo,Bw.Titus Mwisomba,
…………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAKALA wa Umeme vijijini REA kwa kushirikiana na ofisi ya takwimu ya taifa (NBS) wanatarajia kufanya ziara katika mikoa yote nchini kwa ajili ya kufanya tathmini ya watumiaji wa nishati maeneo ya vijijini.
Aidha REA wametumia sh Trion 2.3 kwa ajili ya kuweka Umeme vijijini 8000 kati ya 12,268 vya hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa REA Amos Maganga,amesema kuwa utafiti huo utaangalia tija katika huduma za elimu, maji na uchumi.
Maganga amesema kuwa hadi Oktoba 2019 vijiji 8,000 sawa na asilimia 66 ya vijiji 12,268 vyote nchini vilikuwa vimepatiwa umeme.
Amesema kuwa ziara hiyo itasaidia Wizara ya Nishati kujiridhisha namna ya REA walivyoweka Umeme vijijini ikiwemo kuona matumizi yake.
Hata hivyo Maganga amesema kuwa moja ya mikakati waliojiwekea ni kuhakikisha hadi ifikapo 2021 vijiji vyote vilivyobaki viwe vimefikiwa na Umeme wa REA ili kuboresha maisha ya wananchi.
”Utafiti huu ni muhimu kujua tija iliyopatikana baada ya kusambaza umeme hivyo tunaomba wananchi watoe ushirikiano Kwa wadodosaji ili tuweze kukamilisha zoezi hili” amesema Maganga
Aidha amesema kuwa ziara hiyo itajumuisha watu kutoka Wizara na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ambapo kila mmoja atasimama kwa nafasi yake wakati wa ziara hiyo kuangalia wapi panahitaji kuboresha.
Naye Meneja takwimu za kilimo na mifugo ambaye amemwakilisha mtakwimu Mkuu wa serikali Titus Mwisomba,amesema kuwa wao tayari wameshaanza maandalizi ya vitendo kazi ikiwemo dodoso kwa ajili ya ukusanyaji takwimu.
Mwisomba amesema kuwa kazi ya ukusanyaji wa takwimu itachukua mwezi mmoja na matokeo yatatolewa January 2020.
Aidha amesema kuwa timu ya wataalamu ambayo itatembelea vijiji vyote kwa mujibu wa taratibu zilipangwa na kuongeza kuwa ziara hiyo italeta matokeo chanya.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati Bw.Oscar Kashaigili,amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanajua statasi ya awamu ya tano katika suala la Umeme likoje.
“Tunakwenda katika ziara hiyo ili kujua sekta hiyo ikoje vijijini na sio kuangalia mijini pekeyake na pia watahitaji kuona jamii inapokeaji uwepo wa umeme vijijini,” amesema Kashaigili.