Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano wa kwanza wa kimataifa unaofanyika katika bara la Afrika ukiongelea minyoo ya Tegu ya nguruwe, mkutano wa siku tatu unaofanyika jiji Arusha .(Happy Lazaro).
………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto,Dokta Faustine Ndungulile amesema baada ya tafiti kubaini tatizo la minyoo ya TEGU ya nguruwe kuongezeka kwa kasi hapa nchini na kusababisha athari za afya kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa kifafa,amewatahadharisha walaji wa nyama hiyo kuhakikisha wanakula nyama hiyo na mbogamboga zilizopikwa vizuri.
Dokta Ndungulile ametoa tahadhari hiyo leo jijini Arusha katika
mkutano wa kwanza wa kimataifa unaofanyika katika bara la Afrika ukiongelea minyoo ya tegu ya nguruwe kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja ni jinsi gani nchi hizo zinaweza kutokomeza ugonjwa wa minyoo ya Tegu ya Nguruwe.
Amesema ulaji wa nyama ya nguruwe ambayo ina minyoo ya Tegu ya Nguruwe au mayai,au mbogamboga ambazo zimebeba mayai yaliyotokana na kinyesi cha nguruwe au binadamu ambae ana minyoo tumboni na zikawa hazijapikwa vizuri zinaweza kupelekea magonjwa ya afya ikiwemo kifafa ambacho
hupelekea kifo.
Amesema kuwa,athari zinazoweza kupatikana katika mnyama huyu ni kubwa ikiwemo kupata ugonjwa Wa kifafa , na tatizo hili limeshaingia katika nchi yetu na limeanza kuathiri zaidi katika mikoa ya Manyara,Njombe,Mbeya ,Sogwe ,Mbeya pamoja na mkoa Wa Arusha na asilimia 16%ya wananchi wanaoishi mikoa hii wameshaathirika na ugonjwa huu.
Amebainisha kuwa, hadi sasa serikali yetu haijapata chanjo kwa ajili ya kumzuia mnyoo huyo wa nguruwe na ipo katika utafiti wa kuangalia namna ya kumdhibiti,lakini pia tunaweza kuzuia kwa kuakikisha kuwa tunafuga bila mifugo yetu kuzagaa,pia kwa wale tunaochinja tuhakikishe tumewapima mifugo yetu kwanza bila ya kuwachinja.
Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya magonjwa ya binadamu nchini NIMRI,Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa,kwa hapa nchini wanatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kilimo cha sokoine SUA ambao lengo lake kubwa ni kupata taarifa za kutosha kuhusu tatizo la ugonjwa unaosababishwa na minyoo ya Tegu inayopatikana kwa mnyama nguruwe.
“mradi huu unatekelezwa na nchi zingine mbili afrika ambazo ni
Mozambiq pamoja Zambia na tunashirikiana na wadau wetu wa utafiti wa ujerumani kutoka chuo kikuu cha Munchen ,mradi huu umetuwezesha kununuavifaa vya maabara kwa ajili ya kuweza kufanya utafiti wetuvizuri kwa kiwangoncha juu ,pia umetusaidia kuwapeleka vijana wetu kwenda kupata elimu katika shaghada zauthamini PHD, lakini mradi huu umetuleta pamoja nchi hizi za Afrika na lengo kubwa ikiwa ni kutokomeza au kuzuia watu wasipate ugonjwa huu unaotokana na minyoo hii ya Tegu ”amesema.
Naye Kaimu mkuu wa idara ya tiba ya mifugo na afya ya jamii ambaye pia ni mkurugenzi wa mtandao wa utafiti wa kisayansi Prof,Helena Ngowi amesema kuwa ,mnyoo ni hatari sana kwa sababu anaweza kuleta athari kubwa katika utumbo wa binadamu hadi katika ubongo wa binadamu,anaamini bila ya kuwa na mfugo alie athirika binadamu hawezi kupata ugonjwa huu,pia tafiti hizi zilianza kufanyika tangu mwaka 199 na bado zinaendelea na kiwango cha tatizo kimeshajulikana ,tunashirikiana kwa lengo la kushirikiana katika kupambana na tatizo hili kwa sababu hazina mipaka ,kwa ivyo tunavyoshirikiana na nchi hizi zingine
tunaweza kutokomeza kabisa tatizo hili pia tutashirikisha jamii ili
tuweze kutokomeza.