Kauli hiyo imetolewa Machi 10, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Theopista Mallya ambae alikuwa Mgeni Rasmi kanisani hapo ambapo Wanawake wa Kanisa hilo wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Kamanda Mallya aliwaambia Wanawake hao kuwa wao ni Jeshi kubwa hivyo wanatakiwa kuwa walezi wa familia zao wachunguze na kuchukua hatua pale wanapogundua kwamba kuna matukio ya ukatili, akinukuu kifungu kutoka kwenye Biblia ZABURI 68:11.
Pia, aliwambia Wanawake hao kuwa wao ndiyo wanakaa na watoto muda mwingi hvyo wanapaswa kufundisha watoto Neno la Mungu na kwa kuwa watoto katika umri mdogo wakifundishwa huwa hawasahau, akinukuu MITHALI 22:6. Hivyo mwanamke ahakikishe kwamba yeye sio chanzo cha ukatili, halei ukatili na apaze sauti dhidi ya ukatili.
Vilevile aliwataka Wanawake hao wawe na hulka ya kuongea na watoto wao mara Kwa mara ili kujua changamoto wanazopitia wakiwa nyumbani, njiani au shuleni.
Amewataka Wanawake hao wawe na kiasi akirejea vifungu vya Biblia 2Timotheo 4:5 na 1Petro 5:8 na kuacha manung’uniko na kuridhika na hali walizonazo Kwani hata Mungu hapendi wanaonung’unika kupita kiasi akirejea kitabu cha Hesabu 21:4-8, Kumbukumbu la Torati 8:15 na 1Wakorintho 10:9-13 .
Mwisho amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao mambo matatu, Neno la Mungu, Kazi za mikono na Elimu.