Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Specioza Segesela akiongoza Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kupanda miti katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika eneo la Shule ya Msingi Amani Jijini Dodoma.
………….
Watumishi Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania wameungana na wanawake wengine wa Jiji la Dodoma katika kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani ambayo huadhimishwa Machi 08 kila mwaka.
Maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu “Wekeza kwa Mwanamke: kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa jamii” yamefanyika leo tarehe 08 Machi katika Viwanj a vya Shule ya msingi Chinangali Wilayani Chamwino Jijini Dodoma.
Katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani Wanawake wa TCDC wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi Specioza Segesela wameshiriki zoezi upandaji miti katika Shule ya msingi Amani iliyopo Wilaya ya Dodoma Mjini ikiwa ni kutimiza msingi wa saba wa Ushirika ” Ushirika kujali jamii” katika kutunza mazingira.
Mkuu huyo amesema mazingira yanapotunzwa vizuri hutoa matokeo chanya yanayowezesha Wanawake kuhudumia jamii kwa urahisi na kupata muda wa kuzalisha kipato.
“Mazingira yakiwa mazuri mwanamke anapata muda kuhudumia familia atapata maji karibu, atashiriki kilimo na shughuli nyingine nyingi za uzalishaji”
Akifungua maadhimisho hayo Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia, wanawake na makundi maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa(M b)amesema kuwa; serikali inachukuwa jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa na haki sawa katika nyanja zote na kuondoa umaskini kwa wanawake na wasichana.
“Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa na haki sawa katika nyanja zote, pamoja na kuondoa umaskini kwa wanawake na wasichana na kuanzisha programu mbalimbali za kumuwezesha wasichana kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu ili kumuwezesha mtoto wa kike kuwa mwanamke shupavu na mwenye uwezo” amesema Dkt. Gwajima
Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani kitaifa hufanyika kila baada ya miaka mitano ; kwa upande wa Jiji la Dodoma hufanyika kila mwaka.
Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Specioza Segesela akiongoza Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) kupanda miti katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika eneo la Shule ya Msingi Amani Jijini Dodoma.
Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakishiriki Maandamano ya Siku ya Wanawake Duniani Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma
Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) wakiwa katika Picha ya Pamoja katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Amani wakishiriki na watumishi wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika katika zoezi la Upandaji miti katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Dodoma.