Ferdinand Shayo ,Manyara.
Mshindi wa Mashindano ya Miss Sed 2024 yaliyofanyika Wilayani Babati Mkoani Manyara na kuhudhuriwa na mamia ya Wakazi wa Mikoa Mbali mbali ya Tanzania huku mshindi wa Mashindano hayo mrembo Sara David akinyakua zawadi ya gari jipya aina ya Toyota Vitz new model.
Sara David Mlimbwende aliyetwaa taji ya Miss Sed anaeleza kufuraha yake baada ya kukabidhiwa gari jipya na zawadi ya shilingi milioni moja .
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 19 amesema kuwa urembo ni fursa ambayo inamuwezsha kushiriki katika masula ya kijamii na kiuchumi na kuleta matokeo chanya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo amesema kuwa mbali na zawadi hizo mshindi wa kwanza atapata fursa ya kufanya kazi katika kampuni hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo akifanya vizuri anaweza kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo.
Mulokozi amesema kuwa kampuni hiyo imejifungamanisha na jamii na kuunga mkono masuala mbali mbali ya kijamii ikiwemo mashindano hayo ya Miss Sed 2024 ambayo yanalenga kutoa fursa kwa vijana wa kike.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands limited Gwandumi Mpoma amesema kuwa wamepata mabalozi wa kutangaza kinywaji pendwa kinachozalishwa na kampuni hiyo cha Sed Pineapple flaour gin na pia washiriki wamejipatia zawadi lukuki.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange ameipongeza kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kuwa mstari wa mbele kutoa mchango katika masuala ya kijamii na kiuchumi kwa vijana hususan mashindano hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi.