Mkufunzi Dkt .Kassim Hussein Kassim akiwasilisha mada katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa mfuko wa huduma za Afya huko Ukumbi wa ZSSF Michenzani mall mjini Unguja.
Baadhi ya wajumbe wa mfuko wa huduma za Afya ZHSF wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa mfuko huo huko Ukumbi wa ZSSF Michenzani mall mjini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR
Na Rahma Khamis Maelezo.
Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZSHF) Mbarouk Omar Muhammed amewataka watendaji wa Mfuko huo kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Ameyasema hayo huko Ofisi za Mfuko huo Michenzani Mall wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji na Uongozi wa Mfuko huo.
Amesema kuwa Mfuko huo ni wa kila mwananchi hivyo ipo haja kwa watendaji hao kuongeza bidii zaidi katika utendaji ili kutoa huduma bora na za uhakikakwa wote .
Aidha amefahamisha kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuendeleza huduma za afya ili wananchi wote waweze kupata matibabu kwa gharama nafuu.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia watendaji kupanga mikakati madhubuti itakayopelekea kufanya kazi zao kwa ufanisi ili kuendeleza Mfuko huo na kutoa huduma bora kwa wote.
Mapema kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZSHF Yassin Ameir Juma amesema Mfuko huo bado ni mpya hivyo mafunzo hayo yatasaidia katika utendaji mzuri ili kila mwananchi kupata huduma za afya.
Aidha amewataka watendaji hao kusikiliza kwa makini na kuyapokea mafunzo hayo ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru kupatiwa elimu hiyo kwani itawasaidia katika utendaji wa kazi zao.
Aidha wameaahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa ili kuimarisha afya za wananchi
Hata hivyo wamesea kuwa kupitia mafunzo hayo watahakikisha kuwa kazi zao zinafanyika kwa ufasnisi na kwa haraka
Mafunzo hayo ni ya Siku mbili na yamewashirikisha wakuu wa bodi ya Mfuko pamoja, watendaji na Uongozi