Baadhi ya warembo watakaohudumia wateja kwenye maduka mbalimbali yaliyoorodheshwa kote nchini siku ya ijumaa kwenye ofa ya BLACK FRIDAY.
…………….
- Wateja kurudishiwa hadi 10% ya gharama za malipo siku hiyo.
Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wafanyabiashara mbalimbali nchini imezindua kampeni kabambe inayowawezesha wateja wake kufurahia punguzo kubwa wanapofanya malipo kupitia huduma yake ya M-Pesa. Kampeni hiyo iliyoziduliwa jijini Dar es salaam inalenga kuongeza matumizi ya huduma za kidigitali kwenye kufanya malipo hasa kwenye kipindi hiki cha BLACK FRIDAY, siku maarufu duniani kwa manunuzi ya bidhaa kwenye maduka na mtandaoni.
Kupitia huduma zake mbili za LIPA KWA SIMU na M-PESA MASTERCARD Vodacom M-Pesa wanawawezesha watanzania kufanya malipo kwa wafanyabiashara ndani ya nchi na mitandaoni kupitia simu zao na kurudishiwa hadi 10% ya gharama za malipo siku hiyo ya BLACK FRIDAY ambayo kwa mwaka 2019 itakuwa ijumaa tarehe 29 Novemba.
Meneja masoko wa Vodacom M-Pesa, Noel Mazoya alisema, ‘Black Friday hii tumeandaa ofa ya hadi asilimia 10 ya gharama ambayo wateja wetu watalipa kupitia huduma za LIPA KWA SIMU na M-PESA MASTERCARD. Kupitia huduma ya LIPA KWA SIMU, M-Pesa tutawarudishia hadi asilimia 10 papo hapo wakilipa kupitia mtandao wowote kwenye maduka mbalimbali yaliyopo kwenye malls tofauti nchini. Baadi ya maduka ni kama ifuatavyo kwa Dar es salaam: Mlimani city (Mr Price, Just Fit sports gear, Atsoko, Cassandra Julac, Joo Africa na Vodashop Mlimani, Dar Free Market (Home of events, Zurii house of beauty, Vodacom service desk) City Mall (Kanzu Point, Ley Jewerly, G Best Zone), Rock City Mall Mwanza (Street Soul, Chief Empire Classic, Café Mambo, Upendo Unique beauty shop na Vodashop Rock City) na Aim Mall Arusha (Street Soul, Supa Clean) na mengine mengi. Wauzaji pia watatoa punguzo kabambe la Black Friday.
Meneja uendeshaji wa Mr Price Tanzania Paul Namuhisa alisema ‘Tunafurahi kushirikiana na Vodacom katika kampeni hii. Pamoja na punguzo la hadi asilima 10 ukinunua bidhaa kupitia M-Pesa, Tunatoa punguzo la asilimia 20 kwa manunizi ya bidhaa kwa siku hiyo, huu ni muendelezo wa utamaduni wetu wa kuleta kitu kipya kwa wateja wetu kila siku’
Kwa Upande mwingine, Vodacom kwa ushikiriano na Easybuy Africa itawarudishia wateja hadi asilimia 10 ya kiasi watakacholipa kwa M-PESA MASTERCARD kupitia tovuti ya www.easybuyAfrica.com. Wateja watarudishiwa hadi asilimia 10 wakifanya shopping kutoka mitandao kama Amazon.com, eBay, H&M, Walmart, GAP, Fashionova n.k kupitia EasyBuyAfrica.com na kulipa kwa M-PESA MASTERCARD. Pia watafurahia punguzo la hadi asilimia 10 ya oda zao kutoka EasyBuy pamoja na discount za hadi asilimia 85 kutoka tovuti husika siku ya BlackFriday.
Meneja wa Easybuy Africa, Juliana Siyame alisema, ‘Easybuyafrica inawezesha wateja kununua bidhaa yoyote wanayohitaji kutoka mitandao tofauti duniani na kuwaletea popote walipo Tanzania. Kipindi hiki cha Black Friday tunawawezesha kufurahia huduma zetu kukiwa na punguzo kubwa kwenye bidhaa tofauti pamoja na ofa maalum ya 10% discount wakiagiza nasi ijumaa hii tarehe 29. Ushikiriano wetu na M-Pesa Mastercard umeaongeza faida zaidi kwa wateja wetu kwa kuwapa njia salama ya kulipa mtandaoni’
Wateja ambao bado hawana M-Pesa Mastercard wanaweza kutengeneza kadi zao kwenye menyu ya M-Pesa kwa kupiga *150*00# >Chagua Lipa kwa M-Pesa > Chagua M-Pesa Mastercard kisha > Tengeneza Kadi. Baada ya hapo watapata namba ya kadi, code ya CVV na tarehe ya mwisho wa matumizi, taarifa zinazohitajika kwenye malipo mtandaoni.