Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli akipokea kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Dkt. Danstan Hipolite na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara, Balozi Dkt. Ben Moses hundi ya mfano ya Tzs bil 12.475 ikiwa ni mchango kwa Serikali Kuu wakati wa hafla ya kupokea gawio na michango kutoka mashirika na taasisi za Umma iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 24 Novemba 2019. Kushoto ni Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb).
Rais Dk.John Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi,Mashirika na Kampuni baada ya tukio la kukabidhiwa kwa gawio iliyofanyika leo Novemba 24,Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma