Ndajiri Lonyori kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mchezo wa mpira wa kikapu wa wasichana chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Ndajiri Lonyori kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akionesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa netball chini ya miaka 15 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Amani Isaya kutoka shule ya sekondari Orkeeswa akionesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa volleyball chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Emmanuel Meibuko golikipa wa timu ya shule ya sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mpira wa miguu wa wavulana chini ya miaka 19 baada ya kuibuka washindi kwa goli 3 – 2 katika mechi iliyokuwa ngumu sana kwa vijana hao wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Shule ya Sekondari Orkeeswa iliyopo mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali ya Shule za Kimataifa.
Shule hizo kutoka mikoa mbalimbali nchini zilikutana mkoani Kilimanjaro na kuchuana vikali katika michezo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa miguu, tennis, swimmings, netball, volleyball, frisbie, rugby na michezo mingineyo.
Timu za kikapu U19 wasichana na U19 wavulana pamoja na timu ya mpira wa miguu ya shule hiyo zilionekana kuwa imara zaidi baada ya kushinda kwa kishindo timu za shule mbalimbali zilizo pambana nao.
Shule za kimataifa nchini zilikuwa na wikiendi ya michezo iliyoanza mwishoni mwa wiki,Ijumaa na kufikia tamati Jumapili.