Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wenyeviti wa Chama cha Mapinduzi walioshinda kwa kishindo kwa kupita bila kupingwa katika jimbo la Vwawa Mkoani Songwe jana. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wenyeviti wa Chama cha Mapinduzi walioshinda kwa kishindo kwa kupita bila kupingwa katika jimbo la Vwawa Mkoani Songwe jana.
Sehemu ya Wenyeviti wa Chama cha Mapinduzi walioshinda kwa kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Mbunge wa Vwawa wakati wa kikao kazi kilichofanyika Kata ya Nyimbili Mkoani Songwe jana.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wenyeviti wa Chama cha Mapinduzi walioshinda kwa kishindo kwa kupita bila kupingwa katika jimbo la Vwawa Mkoani Songwe jana.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Serikali imejipanga kuimarisha sekta ya kilimo ikiwa
na dhamira ya kumkomboa mkulima kwa kuimarisha masoko ya bidhaa zao sambamba na
kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za uhakika na kwa wakati.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema hayo jana
wakati akizungumza na wenyeviti wa Chama cha Mapinduzi walioshinda kwa kishindo
kwa kupita bila kupingwa katika jimbo la Vwawa Mkoani Songwe.

Amesema kuwa moja ya mambo ya msingi katika majukumu
yao wenyeviti hao ni kuhakikisha kuwa wanahamasisha wakulima kutumia pembejeo
sahihi wakati wa msimu wa kilimo sambamba na kufuata taratibu bora za kilimo
ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao yao.

Mhe Hasunga alisema endapo wakulima watafuata
maelekezo ya wataalamu mbalimbali wa kilimo wataongeza uwezekano mkubwa katika
uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara jambo litakalopelekea kuimarisha
kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa Wizara ya Kilimo imejipanga vyema
kusimamia upatikanaji wa pembejeo kwa wakati huku akiwahakikishia wakulima kuwa
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itawachukulia hatua za kisheria watendaji wote
watakaoshindwa kusimamia upatikanaji wa pembejeo kwa wakati ili kuendana na
msimu wa kilimo.

Alisema kuwa wapo wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu
ambao wanawauzia wakulima pembejeo feki hivyo amewataka wenyeviti hao
kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa haraka iwezekanavyo kuhusu kadhia hizo punde
wanapopata taarifa kutoka kwa wananchi.

“Waambieni wakulima wote wawe wanatunza mifuko ya
mbegu wanazonunua ili ikionekana hazijaota sisi tushughulike na wote
wanaosambaza” Alisisitiza Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

“Hata shetani alipoasi Mungu alimtupa Duniani pamoja
na kwamba alikuwa muimbishaji mkuu wa kwaya ya mbinguni”

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amepiga marufuku
wafanyabiashara kwenda vijijini na debe la kupimia mazao badala yake wanapaswa
kufuata utaratibu sahihi wa kutumia vipimo vinavyotakiwa ambavyo ni Mizani za
Kidigitali.

Aidha, amewataka wenyeviti kutekeleza majukumu yao
ipasavyo, kutojihusisha na rushwa, na ubadhilifu badala yake amewataka
kuchochea shughuli za maendeleo, kuwa waadilifu, kujituma na kufanya kazi kwa
weledi na uwajibikaji.

Pia Mhe Hasunga amesema kuwa uchaguzi wa serikali za
mitaa umemalizika hivyo amewataka wenyeviti hao kuvunja makundi yote
yaliotokana na uchaguzi ili wananchi wote washiriki shughuli za maendeleo na
kutekeleza kwa ufasaha ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020.