Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza, Elizaberth Nyingi,leo akizungumza na wajumbe wa shina namba 017 la CCM (hapo pichani),Kisesa katika Kata ya Bujora wilayani Magu.
NA BALTAZAR MASHAKA,MAGU
WANAWAKE wameshauriwa kujitokeza kuomba kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu.
Ushauri huo ulitolewa wilayani Magu, na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoani wa Mwanza, Elizabert Nyingi,leo wakati akizungumza na mabalozi wa shina namba 017,Kisesa katika Kata ya Bujora,ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha miaka 47 ya CCM.
Alisema uchaguzi wa serikali za mitaa utakofanyika mapema mwaka huu,wanawake wajitokeze kuomba kugombea nafasi za uongozi kwa kuwa tayari wamepewa kuongoza nchi ili kuwapima kama wanaweza ama hawawezi na majibu yake yanaonekana.
“Tunaongozwa na Mama Jemedari wetu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ameonyesha uwezo mkubwa wa uongozi wan chi na hivyo nawasihi akinamama wenzangu msibaki nyuma,ombeni nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za
mitaa tumuunge mkono Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM,”alisema Nyingi.
Pia alisema wajitokeze kuomba kuchaguliwa na kupiga kura wakishirikiana na wanaume ambao ni ni vichwa vya familia
kuhakikisha CCM inapata ushindi katika uchaguzi wa mwaka ambapo utaonyesha taswira ya kazi aliyoifanya Rais Dk.Samia.
Nyingi alisema wana CCM wanapaswa kuhamasisha wasio na kadi wajiunge na wasajiliwe katika mfumo wa kielektroniki kwa kulipia kadi sh.2,000 na ada ya sh. 1,200 na wawahamasishe hata wa vyama vingine na wasio
na vyama wajiunge na CCM.
“Twendeni tujipange,haya tunayoyafanya ni maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuhakikisha vijiji,vitongoji na mitaa yote CCM inashinda,”alisema Mjumbe huyo wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa hilo namba 017, Felister Mwandu,alisema Rais Samia aliachiwa mzigo mzito wa kuleta
maendeleo ya wananchi akaubeba licha ya kuwa ni mwanamke.
“Tunamshukuru kwa kujitoa na kufanikisha kuleta maendeleo makubwa ya wananchi baada ya kuubeba mzigo alioachiwa,kila mahali ametekeleza ilani ya CCM kwa vitendo.Tunamwombea achape kazi na tunaye pamoja
hatutamwacha,”alisema na kueleza kuwa uhai wa Chama ni wanachama.
Kwa mujibu wa Felister wanafahamu Mama (Rais Dk.Samia), anachapa kazi na Chama kiko vizuri,tatizo liko chini kwa watendaji na wataalamu ndio wanaomkwamisha,wanakwamisha serikali ionekane haifanyi kazi na kushauri kero zinazowakabili wananchi zishughulikiwe haraka.
Mwenyekiti wa Shina la CCM namba 017, Kata ya Bujora wilayani Magu,Felister Mwandu,leo akifungua mkutano wa wa wajumbe (mabalozi) wa shina,walipotembelewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mwanza,Elizaberth Nyingi,kukagua uhai wa Chama na kusikiliza changamoto za wananchi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 47 ya CCM.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mwanza,Robert Nzilanyingi,akizungumza na mabalozi wa shina namba 017 (hawapo pichani),leo Kisesa Kata ya Bujora,Magu baada ya kukagua uhai wa Chama ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 47 ya CCM .
Mwenyekiti wa Mabalozi wa Shina namba 017, Felister Mwandu (wa pili kutoka kushoto),akishauri jambo kabla ya Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza, Elizabeth Nyingi kuzungumza na wajumbe hao.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza, Elizaberth Nyingi,leo akizungumza na wajumbe wa shina namba 017 la CCM (hapo pichani),Kisesa katika Kata ya Bujora wilayani Magu.
Wajumbe wa Shina namba 017 la CCM Kisesa,Kata ya Bujora,leo wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza, Elizaberth Nyingi (kushoto), katika kudhimisha miaka 47 ya CCM.
Thereza Mwehela (kushoto),leo akipokea kadi yake ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza, Elizaberth Nyingi (kulia).
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza,Elizaberth Nyingi,leo akimkabidhi Mjumbe wa Shina namba 017,Rosemary Athanas,kadi yake ya uanachama baada ya kujiunga CCM, Kisesa katika Kata ya Bujora wilayani Magu.