Joctan Agustino-NJOMBE
Mkandarasi anaejenga mradi wa Maji wa Mfumbi wenye thamani ya mil 736 pamoja na Wananchi wa zaidi ya elfu 4,120 kutoka vijiji vya Usalimwani ,Mfumbi na Ruaha vya kata ya Mfumbi iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe wameiomba wizara kumlipa fedha mkandarasi anayetekeleza mradi huo ili aweze kukamilisha ujenzi na watu waondokane na changamoto hiyo iliyowatesa kwa muda mrefu ya kufata maji zaidi ya km 5 mabondeni.
Mradi wa maji wa Mfumbi uliyosainiwa mwanzoni mwa mwaka jana ulikuwa uwe umekamilika mwishoni mwa mwaka jana lakini hadi sasa mkandarasi yupo kwenye uchimbaji wa mitaro jambo ambalo limeibua hisia tofauti kwa wananchi na diwani kwakuwa ni kinyume na mkataba uliyosainiwa wa utekelezaji wa mradi huo katika kipindi cha miezi nane
Akitoa utetezi wake juu ya sababu ya kushindwa kukamilisha mradi huo ndani ya kipindi cha mkataba na kisha kuungwa mkono na wananchi, mkandarasi wa kampuni ya Kizalendo ya HAFRE TECH Haruna Ndanzi amesema ameshindwa kukamilisha mradi ndani ya muda kwasababu ya shida ya upatikanaji wa mabomba pamoja na kucheleweshwa kwa malipo hivyo anaomba kulipwa fedha za mradi zilizosalia na kuongezewa muda wa ujenzi ili kukamilisha kazi kwa ubora unaotakiwa.
“Nimeombe mh Dc nisaidiwe malipo yaliyobaki ili niweze kukamilisha mradi huu na nikutoe shaka nitaumaliza vizuri tu,alisema Ndanzi Mkandarasi”
Mara baada ya kamati ya ulinzi na usalama kukagua na kujionea mkwamo wa mradi huo ndipo mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda akaahidi kuingilia kati suala hilo kwa kumjulisha mkuu wa mkoa ili awasaidie kuwasiliana na watu wa wizara waweze kuleta fedha zote za mradi huo ili ukamilike.
“Mimi nadhani nitasaidia kuwasiliana na watu wa wizara na nitamuomba na mkuu wa mkoa atusaidie ili ziletwe fedha za kumaliza mradi huu na wananchi waanze kupata huduma ya maji safi,alisema Sweda”
Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa wilayani humo Mhandisi Innocent Lyamuya anasema ili kuhakikisha mradi huo unaanza kunufaisha wananchi walimkopesha kiasi cha fedha mkandarasi lakini kwakuwa kilikuwa ni kidogo ni vyema mkuu wa wilaya akasaidia kupata fedha za mradi huo ili mkandarasi aumalizie.
Lyamuya amesema hadi sasa kilichofanyika ni ujenzi wa Mtaro na marekebisho ya tanki la Maji Mfumbi huku kazi nyingine ambazo hazijakamilika ila zipo kwenye mradi ni ununuzi wa pikipiki na kuongeza vituo vya kuchota maji
Aidha Meneja huyo wa RUWASA makete amesema endapo mradi huo utakamilika huduma ya maji wilaya a Makete itakuwa ikipatikana kwa asilimia 100 ambapo kwasasa kiwango cha upatikanaji wa maji ni asilimia 91
“Watu wengi hapa Mfumbi wanachota maji kwenye mifereji mabondeni hivyo kama mradi utakamilika wananchi watakuwa wameondokana na adha hii ya miaka mingi katika eneo hili lenye asili ya ukame,alisema Meneja waRuwasa Innocent Lyamuya”
Nae Diwani wa Kata ya Mfumbi Atilio Ng’ondya anasema wakati serikali ikisaini mkataba wa ujenzi wa mradi huo wananchi waliamini tatizo linakwenda kumalizwa lakini hadi sasa umegeuka kero kwasababu muda wa uetekelezaji umekwisha lakini radi haujakamilika.