Naibu waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Mathew Kundo,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini ulioenda sambamba na kilele cha Maadhimisho ya siku ya Utangazaji Duniani ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika leo Februari 13,2024 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA ) Jones Kilimbe ,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini ulioenda sambamba na kilele cha Maadhimisho ya siku ya Utangazaji Duniani ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika leo Februari 13,2024 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bi.Salome Kessy,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini ulioenda sambamba na kilele cha Maadhimisho ya siku ya Utangazaji Duniani ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika leo Februari 13,2024 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Naibu waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Mathew Kundo,(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini ulioenda sambamba na kilele cha Maadhimisho ya siku ya Utangazaji Duniani ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika leo Februari 13,2024 jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Mathew Kundo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini ulioenda sambamba na kilele cha Maadhimisho ya siku ya Utangazaji Duniani ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika leo Februari 13,2024 jijini Dodoma.
Na.Nestory James-DODOMA
NAIBU Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Mathew Kundo,amevitaka vyombo vya habari kufuatilia kwa umakini mafunzo ya kanuni za uchaguzi katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa kwani vina wajibu wa kutoa taarifa sahihi kwa Wananchi ili uchaguzi Uwe wa amani.
Hayo yameelezwa leo February 13,2024 Jijini Dodoma na Naibu waziri wa Wizara hiyo Kwa niaba ya Waziri wa Habari,Mhandisi Mathew Kundo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini ulioenda sambamba na kilele cha maadhimisho ya siku ya Utangazaji Duniani
Mhandisi Kundo amebainisha kuwa katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vyombo vya Habari vinatakuwa kuwa mstari wa mbele katika kuzingatia Maadili na kanuni za utoaji Habari kwa jamii kwa maslahi ya Taifa.
“Vyombo vya habari vina wajibu mkubwa katika Taifa letu hivyo ni muhimu kila mmoja kuzingatia taaluma na kutimiza majukumu take kwa weledi mkubwa,alisisitiza Naibu Waziri
Pamoja na hayo ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA,kuhakikisha inajitathmini Mara kwa Mara ili kürzt kukuza ni wapi kuna mapungugu na kuweza kufanya kazi mapungugufu hayo.
“Ni muhimu sana kwenu TCRA kuliangalia suala hili kwa umakini mkubwa kwani Mkifanya hivi itawasaidia sana kufanya kazi kwa ufanisi,na Sisi kama Serikali tunawaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuleta maendeleo kwa jamii, “amesisitiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA ) Jones Kilimbe amewataka watangazaji na waandishi wa habari kuzingatia Madili na kanuni ya kazi zao.
Naye Mwenyekiti wa wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini( MOAT)Samwel Nyala amesema pamoja na kukuza tasnia ya habari bado kuna changamoto mbalimbali ikiwemo gharama kubwa ya leseni hali inayowakwambisha na kuwapa hasara ya uendeshaji .
“Tunaiomba Serikali kuangalia suala hilo ikiwa ni pamoja na kuangalia suala la ruzuku kwa Vyombo vya Habari kutokana na kuwepo kwa mdororo wa Uchumi.”amesema Bw.Nyala