Baadhi ya madarasa mapya yaliyojengwa katika sekondari ya Tunduru mkoani Ruvuma
Na Albano Midelo,Songea
SERIKALI imetoa zaidi ya shilingi bilioni 16.7 kujenga miundombinu mipya katika shule za sekondari mkoani Ruvuma.
Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Ruvuma Mwl. Edith Mpinzile amesema fedha hizo zimetolewa katika kipindi cha mwaka 2022/2023 na kwamba zimetumika kujenga sekondari mpya ,mabweni ,nyumba za walimu ,maabara na matundu ya vyoo.
“Ni hakika sasa shule zetu zinang’aa na kupendeza “,alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema serikali ya Awamu ya Sita tangu imeingia madarakani imeweza kujenga shule mpya 20 za Sekondari kwa gharama ya shilingi bilioni 12.74 kupitia Program ya Uboreshaji Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Amesema serikali pia mkoani Ruvuma imeboresha miundombinu ya shule nane za Sekondari ambazo ni Emmanuel Nchimbi, Mpitimbi, Jenista Mhagama, Pamoja, Masonya, Mchoteka,Mataka na Tunduru.
Amesema Mradi huu umehusisha ujenzi wa madarasa 51, mabweni 24 na matundu ya vyoo 93 kwa gharama ya shilingi bilioni 4.45
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas
Baadhi ya madarasa mapya yaliyojengwa katika sekondari ya Tunduru mkoani Ruvuma