Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akijibu swali bungeni leo tarehe 7 Februari, 2024, jijini Dodoma.
Na; Mwandishi Wetu – Dodoma
Serikali imepanga kufanya tathmini ya mafunzo yanayotolewa kupitia programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/25 ili kujiridhisha na ubora wa mafunzo hayo.
Amesema hayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajura na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi leo Februari 7, 2024 bungeni, jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Latifa Juakali, Mbunge wa Viti Maalum, ambaye amehoji, ni kwa kiasi gani Serikali imefanya tathmini ya mafunzo wanayopatiwa vijana nchini kupitia ofisi hiyo baada ya kumaliza mafunzo hayo.
Aidha, Mhe. Katambi amesema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 serikali ilifanya utafiti wa nguvukazi ambapo kiwango cha Ujuzi cha chini kimeanza kuboreka.
Vile vile, Mhe. Katambi amesema kuwa, Serikali imeendelea kuwezesha vijana kupitia programu mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na changamoto ya ajira.