Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan inatarajia kufanya ukarabati Mkubwa wa njia ya reli ya Kati, madaraja na makaravati yote yenye usumbufu kuanzia Dar es salaam mpaka Tabora km 840
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe David Kihenzile wakati wa ziara yake ya kukagua Maeneo ya reli yaliyoharibiwa na mvua zinazoendelea na ukarabati unaofanyika Kwa kutembelea karavati la km 212/3 lililopo eneo la Lukobe kati ya Stesheni ya Morogoro na Mazimbu ambalo liliharibiwa na maji na kukata Mawasiliano na Mikoa mingine lililoko Mkoani Morogoro iliyofanyika Leo Tarehe 2 February, 2024
Mhe Kihenzile amesema Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania Kwa ufadhili wa benki ya Dunia zimeingia mkataba na Mkandarasi mshauri anayeitwa Dohwa JV kufanya usanifu wa kina wa njia ya reli ya Kati, madaraja na makaravati yote yenye mapungufu kuanzia Dar es salaam mpaka Tabora km 840 na kuandaa nyaraka za zabuni kupata Mkandarasi Kwa ajili ya ujenzi chini ya mradi wa TRIP11(Tanzania intermodal Rail Project 11)
“Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuhakikisha Usafiri na usafirishaji Kwa njia ya reli ya Kati unaboreshwa na kuimarishwa ili uweze kutumika vipindi vyote vya misimu ya kiangazi, masika hata kwenye majanga ya mvua kubwa kama hizi za Elnino zinazoendelea” amesisitiza Kihenzile
Awali akitoa taarifa ya kuharibika Kwa miundombinu ya reli Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mha Oswin Matanda amesema kufuatia mvua nyingi zilizonyesha Tarehe 25 Januari,2024 zilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya reli ya kati hasa kuharibika Kwa karavati hili la km212/3 na kusababisha kukatika Kwa Mawasiliano ya Usafiri wa treni kati ya Stesheni ya Morogoro, Mazimbu, na Mikoa mingine
Ameongeza kuwa jitihada nyingi zilifanyika Kwa kushirikiana na uongozi wa juu wa Shirika na ujenzi wa karavati Hilo ulianza Tarehe 26 Januari,2024 na kuisha Tarehe 02 February,2024 Kwa kufanya kazi usiku na Mchana Licha ya uwepo wa mvua nyingi na kufanikiwa kurudisha Mawasiliano ya Usafiri ambayo yataanza kutumika tena kikamilifu hivi Karibuni
Akitoa salami za Mkoa Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini , Katibu Tawala wa manispaa ya Morogoro Bi Ruth John ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi Kwa kuendelea kulisapoti Shirika la Reli Tanzania kifedha hali ambayo imeliwezesha Shirika hilo kushughurikia maafa yaliyojitokeza Mkoani humo Kwa wakati