Na Albano Midelo,Songea 

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaomba wazee wa kimila kusimamia maadili  kwa vijana na familia zao.

Ameyasema hayo, wakati akizungumza katika kikao cha wa wazee wa kimila na Machifu wa Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Amesema vijana wengi wamekosa hofu ya Mungu kutokana na  baadhi ya viongozi  kushindwa kuwajibika katika kutoa maadili mema kwa vijana   hali liyosababisha baadhi ya vijana kuvaa mavazi  yasiyofaa kwa utamaduni wa Tanzania.

“Sisi wenyewe kama wazazi tutimize wajibu wetu wenyewe wa malezi kwa Watoto wetu,tuache kulalamika”, amesema Kanali Thomas.

Kanali Thomas amemeawaahidi wazee hao kuwa atashughulikia changamoto zote wanazokutana nazo wazee zikiwemo ukosefu wa  matibabu, ulinzi  na  kufikisha katika Mamlaka zinazohusika kuhusu ombi lao la wazee wote kupewa pensheni.

Katika kikao hicho Kanali Thomas amewataka matajiri wanao watumikisha watoto katika kazi zao za shambani  waache mara moja  kwa kuwa kuwatumika Watoto ni kinyume cha sheria  zinazomlinda mtoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi Baraza la Wazee Wilaya ya Songea Chrostoms Makukula ameiomba Serikali itoe elimu kwa wazee na kwamba amependekeza wazee wawe na wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama ilivyo kwa wenye ulemavu na wanawake bungeni.

Kwa upande wake Mjumbe Mwakilishi wa Wazee Wanawake Wilaya ya Songea Maria Luoga amewaomba wazee wenzake kukaa na vijana wao ili kuwafundisha maadili mema.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza na wazee kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea 

Baadhi ya wawakilishi wa wazee kutoka Mkoani Ruvuma wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa baada ya kusikiliza kero zap