Na Issa Mwadangala
Amesema baadhi ya vijana ambao ni tegemeo kubwa kwenye jamii katika shughuli za kimaendeleo wanafanya vitendo vya kihalifu ikiwemo kuiba mizigo ya watu iliyopakiwa kwenye magari makubwa yanayoingia ndani ya nchi na yanayotoka nje ya nchi ambayo yanapita kwenye barabra ya Mbeya/Tunduma ambayo imepita kwenye kata hiyo.
“Ni jambo la ajabu kwa kijana ambae ana nguvu za kutosha kushusha mzigo kwenye gari la mtu huku akijua kwamba mzigo huo sio mali yake, lakini nataka mtambue kuwa kufanya hivyo ni kosa na sheria itachukua mkondo wake kwa atakaebainika” alisema mkaguzi huyo.
Aidha aliwasisitiza vijana hao kutumia nguvu zao katika kufanya kazi ili kupata kipato cha halali badala ya kufanya matendo yanayoenda kinyume na sheria ambayo yanaweza kuwaletea athari ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani.
Nao wananchi wa Kata hiyo wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kuwatumia Polisi kata kutoa elimu katika majukwaa mbalimbali nchini.