Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Prof. Siza Tumbo,akizungumza wakati akifungua kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi kutoka ESRF, Vivian Kazi,akitoa taarifa wakati wa kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Afisa Miradi kutoka AGRA, Liston Njoroge,akiongea wakati kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya usalama wa chakula kutoka wizara ya kilimo Dkt.Honest Kessy,akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Prof. Siza Tumbo,ambaye alifungua kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Prof. Siza Tumbo,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Prof. Siza Tumbo amesema taarifa rasmi ya Benki ya Dunia zinabainisha kuwa tayari Tanzania imeshafikia uchumi wa kati.
Prof.Tumbo ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo.
Amemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kufikia na kujikita kwenye uchumi wa kati.
“Sasa hivi Tanzania tunachukuliwa kama hatujafikia uchumi wa kati, naomba wataalam wetumjue kwamba tumeshafikia uchumi wa kati sasa hayo maandishi kuwa tuna mpango wa kufikia uchumi wa kati naomba mbadili, taarifa rasmi ya benki ya Dunia imeshasema Tanzania ipo kwenye uchumi wa kati isipokuwa hatujajikita katikati ya uchumi wa kati ndo tofauti.”amesema.
Hata hivyo, amebainisha kuwa kuna wakati Tanzania iliingia uchumi wa kati lakini ikatereza na kwasasa imerudi tena na kwamba uwezekano wa kuteleza ni mdogo.
“Kwasababu hizo napenda kumshukuru Rais John Magufuli kwa kuweza kutuingiza kwenye uchumi wa kati na tunaendelea kujikita kwenye uchumi wa kati, sasa hivi ukuaji wa uchumi kwenye upande wa kilimo sasa hivi tumefikia asilimia 5.3 na lengo ni asilimia 6 kwa hiyo tayari tunakwenda kwa kasi,”amesema.
Prof.Tumbo amesema kwa mwaka huu Tanzania imefikia asilimia 109 ya utoshelevu wa chakula kwa kuwa na ziada ya chakula tani milioni 2.5.
Akizungumzia kuhusu uuzaji mazao nje ya nchi, Prof.Tumbo amesema kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu, Tanzania imeuza nchini Burundi mihogo tani 5,000 Burudi, tani 2000 za mtama na mahindi tani 84,000.5.
“Kwa kuwa tunahamasisha mabadilishano ya kibiashara tumeingiza mahindi tani 56000.4, kwa hiyo kimahesabu jumla ya tani zilizoenda nje ni tani 28,100 unaposema kwamba unataka ku encourage trade ni pamoja na watu kuingiza vitu kwako na wewe kupeleka nje ya nchi, mchele ndo tumeingiza kidogo sana tani 20,”amesema.
Kadhalika, amesema zao kubwa linaloingizwa ndani ya nchi ni ngano kutokana na uzalishaji kuwa chini.
Kwa Upande wake,Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi kutoka ESRF, Vivian Kazi amesema wamefanya kazi nyingi za kitafiti na kwamba zinalenga kusaidia kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa pamoja na kuboresha usalama wa chakula kwa kupitia usimamizi bora na madhubuti.
Amesema malengo ya mradi wa tafiti hizo ni kuboresha upatikanaji wa taarifa,kuboresha mahusiano ya kiutendaji na taasisi muhimu zenye majukumu ya kusimamia usalama na biashara chakula,kuimarisha taratibu za tathmini za chakula ili kuboresha makadirio kwa kuzingatia matokeo ya vipimo.
Naye, Afisa Miradi kutoka AGRA, Liston Njoroge amesema wataendelea kushirikiana na taasisi hiyo na serikali kufanya tafiti nyingi zaidi kwenye masuala ya kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi ili kuleta tija kwa Taifa.