Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa mgeni wa heshma katika Hafla ya Chakula cha usiku na Taarab katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar jana katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Makamo wa Rais wa Burundi Mhe.Prosper Bozombaza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa (katikati) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdalla (wa pili kushoto) Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Mhe.Abdulrahman Kinana (kushoto) Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Doto Biteko na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman wakiwa katika hafla ya Taarab rasmi na chakula cha Usiku katika viwanja vya Ikulu jana katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi na waalikwa mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya Chakula cha usiku na Taarab katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar jana katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Ranzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiagana na Makamo wa Rais wa Burundi Mhe.Prosper Bozombaza wakati wa kumalizika kwa Hafla ya Chakula cha usiku na Taarab katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar jana katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na Viongozi wengine wakienda kutunza wakati Vikundi vya Taarab vilipotumbiza jana Ikulu katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Ranzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi baada ya kumaliza kwa hafla ya Chakula cha usiku na Taarab katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar jana katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Kikundi cha Taarab cha Taifa cha Muzicul Club wakitumbiiza Chakula cha usiku na Taarab katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar jana katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. [Picha na Ikulu.