IBRAHIM JERA MAISHA KWA KOSA LA KUBAKA-Songwe.
Na Issa Mwadangala
Mahakama ya wilaya ya Momba imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha maisha Gerezani mshitakiwa Ibrahim Salum (35) Dereva wa bajaji kwa kosa la kubaka.
Ibrahim alikamatwa Januari 28, 2023 maeneo ya Maporomoko, tukio hilo alilifanya kwa kumlaghai mwanafunzi wa darasa la 3 mwenye umri wa miaka 9 kwa kumwambia atamnunulia chips kisha kumvuta karibu na nyumbani kwake kwenye nyumba ambayo aijaisha na kutekeleza kitendo hicho.
Akitoa hukumu hiyo Disemba 18, 2023 kwa kesi namba 83 ya mwaka 2023 Mheshimiwa Hakimu mkazi wa wilaya ya Momba Kannonyele amesema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.
Mshtakiwa amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto.