Mkuu wa idara ya huduma za kiufundi na Kinga za mionzi katika Taasisi ya nguvu za atomu Tanzania TAEC Yesaya Sungita akizungumza katika mkutano huo mkoani Arusha.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini semina hiyo inayoendelea mkoani Arusha.
Julieth Laizer,Arusha .
Arusha .Taasisi ya tume ya nguvu za atomu Tanzania TAEC imeandaa mafunzo ya siku Tano katika ofisi ya Kanda ya kaskazini iliyoko njiro mkoani Arusha kwa madaktari wanaotoa huduma za mionzi nchini lengo likiwa ni kuhakikisha usalama eneo la kazi pamoja na wagonjwa wanaopatiwa huduma ya mionzi katika teknolojia ya nyuklia.
Akizungumza mara baada ya kufungua mafunzo hayo Mkuu wa idara ya huduma za kiufundi na Kinga za mionzi katika Taasisi ya nguvu za atomu Tanzania TAEC Yesaya Sungita amesema lengo kuubla mafunzo hayo ni kutoka elimu juu ya usalama wa matumizi ya mionzi pamoja na kujua namna Bora ya kuwakinga wagonjwa dhidi ya mionzi.
Aidha Sungita aliongeza kuwa mafunzo hayo pia yanatoka elimu juu ya jinsi ya kujikinga na jinsi ya kutumia teknolojia ya nyuklia katika huduma mbalimbali katika Hali ya usalama ili kuhakikisha kwamba watanzania wanalindwa wasiweze kupata madhara kulingana na matumizi ya teknolojia ya nyuklia.
Amesema kujikinga kunaanzia kwa mtoa huduma lazima ajue mbinu za kiusalama za kuweza kujikinga na pia aweze kumkinga mgonjwa asiweze kuathirika na mionzi ya nyuklia na mionzi inatumika sehemu mbalimbali ikiwemo kutoka huduma za tiba pamoja na uchunguzi wa magonjwa.
Pia amesema wao kama tume wanamatarajio makubwa kupitia mafunzo hayo kuwa madaktari hao pindi watakapo Rudi sehemu zao za kazi wataweka usalama utaimarika kwa kuwa wap ni washauri wa menejimenti kulingana na matumizi ya mionzi katika eneo lao na watakuwa na uwezo wa kutoka usharudi kwamba ni hatua Gani inaweza kuchukuliwa ili kuhakikisha kwamba usalama unaimarika na wagonjwa wanapata huduma sahihi na kwa wakati stahiki.
Daktari kutoka hospitali ya wilaya ya Rombo,Alfred Nzele amesema wameshiriki mafunzo hayo lengo likiwa ni kupata elimu juu ya usalama wa matumizi ya mionzi ili kujua namna Bora ya kuwakinga wagonjwa dhidi ya mionzi.
Amesema kuna umuhimu mkubwa wa mafunzo hayo kwani mionzi inatumika katika njia nyingi na wao wako kwenye kitengo Cha kuchunguza na kutibu na mafunzo haya yatawasaidia kwenda kutoka huduma nzuri na yenye ueledi kwa wagonjwa.
Naye Sister Marietha Kurwa kutoka hospitali ya singida amesema mafunzo hayo yatawanufaisha kwa namna Moja Hadi nyingine na wataenda kufanyia kazi elimu waliyopatiwa kwa ajili ya kumlinda mgonjwa ,kumesaidia mgonjwa kupata huduma Bora pamoja na kumlinda mwenyewe kutokana na mionzi na teknolojia hiyo wataitumia vizuri .