Baadhi ya maafisa wa ulinzi na usalama, viongozi wa chama na Serikali pamoja na wananachi wa mkoa wa kaskazini Pemba wakiwa katika hafla ya kujadili fursa na mbinu za kuzifikia katika mkoa huo, huko Ukumbi wa baraza la wawakilishi Wete Pemba.
Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarok Khatib akizungumzia kuhusiana na fursa zilizomo katika Mkoa wakena mbinu za kuzifikia ,huko Ukumbi wa baraza la wawakilishi Wete Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Micheni Mgeni Khatibu Yahya akifanya mahojiano na mwandishi wa habari ZBC Salum Othman kuhusiana na fursa zinazopatikana katika wilaya hiyo,huko Ukumbi wa baraza la wawakilishi Wete Pemba.
Mkurugenzi halmashauri wilaya ya micheweni Hamadi Mbwana Shehe akifanya mahojiano na mwandishi wa habari ZBC Salum Othman kuhusiana na fursa zinazopatikana katika halmashauri hiyo,huko Ukumbi wa baraza la wawakilishi Wete Pemba.
Mwenyekiti wa Baraza la vijana Wilaya ya micheweni Ishak Khamis Shame akichangia katika hafla ya kujadili fursa na mbinu za kuzifikia ndani ya mkoa wa Kaskazini Pemba , huko Ukumbi wa baraza la wawakilishi Wete.
Amour Saleh Said mkaazi wa Kipangani akichangia katika hafla ya kujadili fursa na mbinu za kuzifikia ndani ya mkoa wa Kaskazini Pemba , huko Ukumbi wa baraza la wawakilishi Wete.
Amour Rashid Amour mkaazi wa Mwane kaskazini Pemba akichangia katika hafla ya kujadili fursa na mbinu za kuzifikia ndani ya mkoa wa Kaskazini Pemba , huko Ukumbi wa baraza la wawakilishi Wete.
Mkuu wa chuo cha mafunzo ya TEHAMA Limbani (WHYDAH) Salum Mohammed Ali akichangia katika hafla ya kujadili fursa na mbinu za kuzifikia ndani ya mkoa wa Kaskazini Pemba , huko Ukumbi wa baraza la wawakilishi Wete.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na Fauzia Mussa-Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na wadau inaendelea na harakati za kukamilisha ujenzi wa Ghala eneo la Taifu kaskazini Pemba ili kupunguza gharama kwa wafanya biashara wanaochukua bidhaa nje ya Nchi.
akizungumzia fursa za Mkoa wa kaskazini Pemba huko ukumbi wa Baraza la wawakilishi wete Mkuu wa mkoa huo Salama Mbarok Khatib amesema kukamilika na kufunguliwa kwa ghala hilo linalobeba tani elfu 7 kutatoa fursa za ajira kwa vijana na kupunguza ukali wa maisha .
Amesema katika mkoa wa kaskazini Pemba akinamama wengi wamekuwa wakinufaika na kilimo cha mwani , na kuwataka kuendeleza kilimo hicho kwa fursa zaidi zinazotokana na uchumi wa Buluu.
Aidha alisema wananachi kwa ujumla katika Mkoa huo wananufaika na fursa za kilimo katika zao la karafuu na mazao ya chakula ili kumiliki mlo na kupata kipato cha mtu mmojammoja na taifa kwa ujumla .
Aidha kupitia fursa za elimu katika Mkoa huo Mhe. Salama alisema wataalamu wa fani mbalimbali wanawawezesha vijana kujiajiri na kuweza kuajirika.
Kuhusu suala la Viwanda na nishati ya umeme amesema kiwanda cha maji cha Kinyikani na Chamanangwe vinaendelea kutoa ajira kwa vijana ,pamoja na kuitumia vyema fursa ya upatikanaji wa umeme kisiwani humo ili kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi.
Amesema barabara zinazoendelea kujengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Visiwani humo zimekua zikitoa fursa kwa vijana kuweza kujiari katika usafirishaji wa abiria ardhini na kujikomboa kiuchumi pamoja na kuwarahisishia wakulima kuweza kuyafikia masoko kwa wepesi na kuuza bidhaa zao.
Kwa upande wake Afisa mdhamini wizara ya biashara na viwandaa Ali Sleiman Abeid amesema Serikali imewekeza kujenga kiwanda kikubwa cha kusarifia mwani eneo la Chamangwe kinachohitaji tani elfu 30 kwa mwaka na kutoa fursa za ajira hivyo aliwataka wakaazi wa mkoa huo kuendeleza harakati za kilimo hicho ili kuzikimbilia fursa zinazotokana na uchumi wa buluu na kufikia malengo ya Serikali kupitia fursa hizo.
Afisa Mratibu Wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi (ZEEA) Haji muhammed Haji amesmea jumla ya shilingi bilioni 5 zimewekezwa na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika Benki ya CRDB ili kuwawezesha wananachi kiuchumi ,hivyo aliwataka kuchangamkia fursa ya Mikopo inayoenda kuhuisha shughuli za vijana ikiwemo ujasiriamali na biashara.
Aidha alifahamisha kuwa bado vijana wengi mkoani humo hawana muamko wa kuzichangamkia fursa zilizopo na kuwahamasisha kujitokeza kuchukua mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa
Washiriki wa mkutano huo wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa fursa hizo za maendeleo na kuwataka wanaochukua mikopo kuitumia katika madhumuni yaliyokusudiwa na kurejesha kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika nayo .
Hata hivyo waliiomba ZEEA kutowa elimu zaidi kwa vijana kwani wengi wao wamekuwa na woga wa kuchukua mikopo hiyo kutokana na uelewa mdogo juu ya mikopo hiyo.
Mkutano huo uliowakutanisha wananchi wa Mkoa wa Kaskazini pemba,Mkuu wa Mkoa huo na Wadau wa uwekezaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi ulilenga kuangazia fursa zinazopatikana katika Mkoa huo na mbinu za kuzifikia.