Mratibu wa Mradi wa USAID Boresha Afya (EGPAF) Halmashauri ya Singida MC/ Singida DC na Ikungi, Nicholaus Njoka, akizungumza kwenye kikao cha Wadau cha robo mwaka cha Tathmini ya Hali ya Ukimwi mkoani Singida jana.
Wadau wa Sekta ya Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau wa Sekta ya Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wadau wa Sekta ya Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau wa Sekta ya Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Mfamasia wa Mkoa wa Singida, Joseph Mwasambili akizungumza kwenye kikao hicho.
Wadau wa Sekta ya Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Shughuli za VVU/ UKIMWI Ngazi ya Mkoa wa Singida, Dkt. Mohammed Mbalazi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Wadau wa Sekta ya Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Meneja Mkoa wa Singida wa Kampuni ya Tutume, Nuru Tamimu, akitoa mada katika kikao hicho.
Afisa wa Huduma za Maabara Mkoa wa Singida, Musa Msiganga, akichangia jambo.
Meneja Mwandamizi kutoka USAID Boresha Afya (EGPAF), Charle Makoko, akitoa mada kwenye kikao hicho.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SABABU kadhaa zikiwemo mwingiliano mkubwa wa watu na maboresho ya miundombinu zimetajwa kama chachu inayochagiza ongezeko la maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Singida, imeelezwa
Kwa mujibu wa tafiti ya 2016/2017 ijulikanayo kama ‘THIS’ (Tanzania HIV/AIDS Indicator Survey) imebainisha kuwapo kwa ongezeko la kiwango cha maambukizi hayo na kufikia asilimia 3.6 sawa na ongezeko la asilimia 0.3 kwa sasa, ikilinganishwa na asilimia 3.5 kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa kwa mara ya mwisho mwaka 2012.
Mratibu wa shughuli za VVU/UKIMWI mkoani hapa, Dkt. Mohamed Mbalazi, alisema pamoja na mambo mengine, ongezeko hilo linachagizwa na mwingiliano wa watu ambao umetokana na matumizi ya miundombinu ya barabara zinazokatisha ndani ya mkoa wa Singida.
Alisema mbali ya njia hizo za usafirishaji sababu nyingine ni ongezeko la maeneo ya starehe na baadhi ya watu ndani ya jamii kuendekeza ngono zembe-bila ya kuchukua tahadhari yoyote ya kujikinga ikiwemo kutozingatia matumizi ya condom.
Alisema kusanyiko hilo la wadau na wataalamu ni mwendelezo wa vikao vinavyofanyika kila robo ya mwaka lengo hasa ni kupitia takwimu za VVU/UKIMWI, hususani kwenye maeneo ambayo yanaonekana kuwa na idadi kubwa ya wateja wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI
Alisema tathmini hiyo ya siku 2 ililenga kuangalia ni kwa namna gani utekelezaji wa mpango mkakati na malengo waliyojiwekea kati ya Julai na Septemba kama yamefikiwa ipasavyo
“Kwahiyo kwa robo hii wadau wote tumekutana hapa kufanya tathmini na kupitia ripoti mbalimbali kwa maana ya kujiridhisha wapi tumefanikiwa na wapi bado kuna changamoto na namna ya kukabiliana nazo,” alisema Mbalazi
Mbalazi alisema washiriki waliopo wanatoka katika halmashauri zote saba za Itigi, Manyoni, Ikungi, Singida DC, Singida Manispaa, Mkalama na Iramba pamoja na wataalamu wa timu ya afya ya mkoa wa Singida.
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa USAID-Boresha Afya ambao wamekuwa wakijitambulisha kama Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) wamekuwa mstari mbele katika kuleta ustawi wa afya ya jamii hususan eneo la mapambano dhidi ya Ukimwi.