Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi jana mkoani hapa. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Alhaji Chima Mbua na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili.
Mtahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Alhaji Chima Mbua, akiongoza kikao hicho. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bravo Lyapembile.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili, akizungumza kwenye kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdamu, akiuliza swali kwenye kikao hicho. Kulia ni Diwani wa Viti Maalumu, Margaret Malecela na Diwani Hadija Simba.
Madiwani wakifuatilia kikao hicho kwa umakini.
Watendaji na wakuu wa idara wakiwa kwenye kikao hicho.
Vijana wa Kikundi cha Familia Moja, wakionesha mikate wanayoitengeza baada ya kuwezeshwa na Manispaa hiyo. Kutoka kulia ni Katibu wa Kikundi hicho, William Mollel, Mweka Hazina, Bonaventure Njiku, Katibu Msaidizi, John Chacha, Mjumbe wa Kikundi, Cleophace Okulo na Mwenyekiti, Benard Mahenge.
Diwani wa Kata ya Unyami, Said Athuman , akizungumza kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Kisaki, Moses Ikaku , akizungumza kwenye kikao hicho.
Naibu Meya, Shabani Mkata, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Lucia Mwiru, akizungumza kwenye kikao hicho. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Shabani Karage.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida kwa mwezi wa Oktoba 2019 imefanikiwa kukusanya sh.milioni 248,858, 234.12 za mapato.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilicho keti mjini hapa jana baada ya kupata nafasi ya kuzungumza.
” Napenda kuwapongeza kwa ukusanyaji huu wa mapato tuna kwenda vizuri na tupo ndani ya wastani wa kila mwezi wa ukusanyaji wa mapato yetu” alisema Muragili.
Alisema kwa siku 14 zilizopita hadi kufikia jana saa nne asubuhi halmashauri hiyo imeweza kukusanya sh.milioni 72.594,308.06.jambo ambalo linaashiria kuwepo kwa kazi nzuri ya kukusanya mapato.
Muragili alisema mpaka Oktoba 31 mwaka huu halmashauri hiyo ilikuwa na zaidi ya sh milioni 190 zilizokuwa nje kama madeni lakini kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa deni hilo limepunguzwa hadi kufikia sh.64.6 milioni ambapo aliomba ziongezeke juhudi waweze kulipunguza hadi lifikie sh.milioni 10.
Katika hatua nyingine Murigili amewata madiwani wa halmashauri hiyo katika kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha kwenda kwa wananchi kuwahimiza kilimo si kwa mazao ya chakula pekee bali walime na mazao ya kimkakati pamba, korosho na zao linalochukua alama ya mkoa wa Singida la alizeti.
Murigili alitumia nafasi hiyo kuwaomba madiwani hao kwenda kuwaeleza wananchi wao kutouza chakula walichokihifadhi baada ya bei katika soko kwa hivi sasa kupanda kwani kuna viashiria vya uhaba wa chakula kati ya Januari na Februali.
Katika suala la utunzaji wa mazingira aliwataka madiwani hao mbali na shughuli za kilimo waende kuhimiza upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali na kwenye maeneo ya taasisi kama za shule na ofisi za serikali.
Akizungumzia maandalizi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2020 alisema mwaka jana waliingia katika mchakato wa kutengeneza madawati hivyo aliiomba halmashauri hiyo kujipanga katika jambo hilo ili msimu wa masomo utakapoanza vijana hao wakae kwenye madawati.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bravo Lyapembile akizungumza kwenye kikao hicho wakati akiwakaribisha vijana wajasiriamali wa kikundi cha Familia Moja waliowezeshwa na manispaa hiyo kwa kukopeshwa sh.milioni 10 kwa ajili ya mradi wa kutengeneza mikate na maandazi alisema halmashauri imetenga zaidi ya sh.milioni 100 kwa ajili ya kusaidia vikundi mbalimbali na alitumia nafasi hiyo kuwaomba waliokopa kurejesha fedha kwa wakati ili ziweze kukopeshwa kwa vikundi vingine.