Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na Wananchi wa Kusini (hawapo pichani) kuhusiana na fursa zilizomo Mkoani humo na njia ya kuzifikia katika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar .
Baadhi ya Vijana wa Mkoa wa Kusini Unguja wakisikiliza fursa zilizomo katika Mkoa wao wakati zikielezewa na Mkuu wa Mkoa huo Ayoub Mohammed Mahmoud (hayupo pichani ) huko Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar.
Baadhi ya Wazee wa Mkoa wa Kusini Unguja wakisikiliza fursa zilizomo katika Mkoa wao wakati zikielezewa na Mkuu wa Mkoa huo Ayoub Mohammed Mahmoud (hayupo pichani ) huko Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar.
Mwananachi wa Mkoa wa Kusini Unguja Ibrahim Haji Juma akiuliza swali wakati wa mkutano wa wakuelezea fursa zilizomo katika Mkoa huo na namna ya kuzifikia uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar.
Mkalimani wa lugha za alama Khadija Ali Ame akiwasaidia uelewa watu wenye ulemavu wa uziwi wakati wa mkutano wa wakuwasilisha fursa zilizomo katika Mkoa wa Kusini Unguja na namna ya kuzifikia uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi Serikali ya Wanafunzi SUZASO Laurant Mwita Mahemba akiuliza swali wakati wa mkutano wa kuwasilisha fursa zilizomo katika Mkoa wa Kusini Unguja na namna ya kuzifikia uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar.
Waziri mteule Wizara ya Maendeleo na Uwezeshaji kwa watu wenye Ulemavu SUZASO Nassir Salum Ali akiuliza swali kuhusiana na fursa za wanafunzi wenye mahitaji maalum wakati wa mkutano wa wakuwasilisha fursa zilizomo katika Mkoa huo na namna ya kuzifikia uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar.
Mwananchi wa Shehia ya Kizimkazi Mkunguni Rahma Kassim Mtawa akiuliza suali kuhusiana na fursa za watu wenye ulemavu wasioona wakati wa mkutano wa wakuwasilisha fursa zilizomo katika Mkoa huo na namna ya kuzifikia uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na Ali Issa na Mwashungi Tahir wa Maelezo.
Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud amesema Mkoa wa kusini unafursa nyingi za kimaendeleo ambazo wananchi wake wanapaswa kuzichangamkia frusa hizo ili waweze kujipatia Maslahi katika maisha yao.
Ameyasema hayo leo Tunguu katika ukumbi wa Dkt. Ali Muhamed Shein katika kipindi cha Mkono kwa Mkono kinachoendelea katika Mikoa yote ya Zanzibar kufuatia maadhimisho ya sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema fursa hizo ni pamoja na uwekezaji mkubwa wa Hoteli, vyuo vikuu vitano, kilimo, ufugaji, uvuvi na Barabara.
Amesema iwapo maeneo hayo watayatumia vyema ipasavyo mkoa huo utapiga hatua kubwa ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za kupambana na ugumu wa kimaisha.
“Mkoa huu una Hoteli nyingi zinahitaji bidhaa za mbogamboga,matunda na samaki vituambavyo vinapatikana kwa wingi mkoani humu kama tutaimarisha bidhaa hizi vizuri basi changomoto ya kupambana na ukali wa maisha utaisha,”alisema Ayuob.
Alisema wananchi walime sana bidhaa zinazo hitajika ikiwemo matikiti na mbogamboga nyengine pamoja na kuendeleza uvuvi wa kisasa wa kutumia Maboti yaliotolewa na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi katika Mkoa huo.
Aidha alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeelekeza nguvu zake kwa kuwainua kiuchumi vijana kwa kuwaezesha katika nyanja mbalimbali, kupewa mikopo nafuu isio na riba hivyo vijana wasibweteke wawe tayari kufuata mikopo hiyo kwa kutimiza masharti yalio wekwa na Serikali ili wafaidike na matunda ya Mapinduzi.
Hatahivyo alisema kuwa Serikali ipo tayari kujenga Mabweni ndani ya chuo ili kuepusha udhalilishaji kwa wanafunzi wa kike.
Hata hivyo aliwataka wanafunzi wa kike wawafichue walimu wanao wadhalilisha chuoni na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mwalimu atakaekuwa hana nidhamu.
Mkurugenzi mafunzo uwezeshaji wananchi kiuchumi Fatma Muhamed Juma amesema wao hutoa mafunzo kuwasaidia wajasiriamali,kuwatafutia masoko pamoja na kuwapa mikopo ya kuendeleza biashara zao wanazo zifanya.