Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Yasir Ameir Juma akitoa elimu kwa watendaji wa Wizara ya Elimu katika muendelezo wa kujenga uwelewa wanachama wake juu ya dhana ya mfuko huo huko Ofisi za WEMA Mazizini Zanzibar.
Afisa kutoka Wizara ya Elimu Asha Makame akiuliza swali wakati wakipatiwa elimu juu ya dhana ya mfuko wa huduma za Afya huko Ofisi za Wema Mazizini Zanzibar.
Afisa kutoka Wizara ya elimu Asha Kesi akiuliza swali wakati wakipatiwa elimu juu ya dhana ya mfuko wa huduma za Afya huko Ofisi za Wema Mazizini Zanzibar.
Afisa kutoka Kitengo cha Takwimu Wizara ya Elimu Ibrahim akiuliza swali wakati wakipatiwa elimu juu ya dhana ya mfuko wa huduma za Afya huko Ofisi za Wema Mazizini Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
NA FAUZIA MUSSA, MAELEZO
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Yasir Ameir Juma amewataka wanachama kuendelea kuchangia na kuulinda Mfuko huo ili kuwanufaisha siku hadi siku.
Akizungumza na watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar katika muendelezo wa utoaji wa elimu kwa wanachama wake huko Mazizini kaimu huyo alisema utaratibu huo utauwezesha kuendelea kutoa huduma Bora za Afya kwa wote .
Amesema kila mmoja ana haki ya kuchangia katika mfuko huo kulinagana na uwezo wake na Serikali itabeba jukumu la kuwachangia wasiokuwa na uwezo ikiwemo mayatima na wanafunzi wa Chuo cha mafunzo.
“lengo la kuchangia katika mfuko huu ni kujiwezesha kupata rasilimali zetu wenyewe za kuweza kutengeneza mazingira na kuhakikisha tunazalisha miundo mbinu yetu wenyewe ya huduma za Afya na mwisho wa siku tuone watu wanatoka nje ya Zanzibar kufata Huduma Bora ndani ya Nchi yetu .” Alisema Kaimu huyo
Amesema Zanzibar ni Nchi ya pili kwa Afrika Mashariki kufikia adhma ya Afya Bora kwa wote hivyo aliwataka wanachama hao kuendelea kuutunza kwa maslahi ya Taifa.
Alifahamisha kuwa Misingi iliotumika kuanzisha mfuko huo ni kutengeneza umoja pamoja na kusaidiana katika kupata huduma hizo kwa usawa.
Awali aliwataka wanachama hao kuwa watulivu kusibiri kundi la watu wengine kusajiliwa na kupata huduma kupitia mfuko huo wakiwemo watoto wakulea sambamba na kuwataka kupeleka taarifa na changamoto zinazojitokeza wakati wa upatikanaji wa huduma hizo sehemu husika ili kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Kwa upande wake Afisa Usimamizi Ubora wa Huduma za Afya ZSHF Dkt. Habiba Sultan Mbwana amevitaka vituo vinavyotoa huduma kupitia mfuko huo kuwapatia huduma stahiki wanachama wake bila usumbufu wowote.
Amesema mfuko umeweka utaratibu wa kuanzia katika zahanati ili kupunguza wimbi kubwa la wagonjwa katika hospitali za Rufaa.
Nao washiriki wa mafunzo hayo waliwaomba watendaji wa ZSHF kuendeleza kutoka elimu ili lengo liweze kufikiwa kwa haraka.