Na Eleuteri Mangi, WUSM
Tanzania ni mwenyeji wa tamasha la dunia la watu wenye usikivu hafifu (viziwi) likihusisha shindano la kumsaka mrembo, mtanashati pamoja na wanamitindo litakalofanyika Novemba 25, 2023 jijini Dar es salaam.
Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi amesema maadalizi yanaendelea vizuri na Tanzania imejipanga kufanikisha tamasha hilo ambalo Tanzania imepewa heshgima ya kuwa mwenyeji kwa miaka miwili mfululizo.
Maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vyema kwa washiriki kujinoa ili kutoa taji la urembo, utanashati pamoja na wanamitindo dunia kwa viziwi ambapo mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya pili mfululizo hapa nchini baada ya kufanyika kwa mara ya kwanza Afrika na Tanzania kwa 2022.
Hadi sasa washiriki zaidi ya 200 wa tamasha hilo wameshawasili tayari nchini wanatoka mataifa ya Afrika Kusini, Australia, Belarus, Brazil, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Guyana, Haiti, Hispania, India, Iran, Italia, Kenya, Kongo DRC, Malasia, Macedonia, Marekani, Mexico, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Pakistan, Poland, Romania, Rwanda, Senegal, Siera Leone, Sudan Kusini, Thailand, Tunisia, Jamhuri ya Czechoslovakia, Ufaransa, Uganda, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.