Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wizara ya Maji, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga wameendesha mafunzo kwa Wasimamizi wa Vyombo Vya Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) Mkoa wa Shinyanga kuhusu kuhamisha Taarifa za CBWSOs) kwenda kwenye Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki (GePG) kupitia Mfumo wa Maji’s Billing System and Government Collection Platform) ambao utasaidia kuendesha miradi ya Maji Vijijini kwa tija.
Akizungumza leo Jumatatu Novemba 20,2023 katika ukumbi wa Hash Mjini Shinyanga wakati wa kufungua mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku 10, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako amesema mafunzo hayo yatawajengea uelewa wa kutosha juu ya Mfumo wa Malipo kwa njia ya Kielekroniki na kuondoa changamoto za Makusanyo ya fedha za maduhuli ya mauzo ya Maji maeneo ya Vijijini.
“Katika kipindi cha siku kumi mtajifunza mada mbalimbali zitakazowaongezea ufanisi katika utendaji kazi wenu kwenye Sekta hii ya maji. Kupitia mafunzo haya mtahamisha taarifa zote za wateja wa Maji kwenda kwenye Mfumo wa Wizara ya Maji – Majis. Pia mtakuwa na uwezo wa kusoma, kuandaa na kusambaza ankara za Maji kwa wateja wenu pamoja na kulipia Ankara za Maji kwa kupitia Mfumo wa Malipo wa Kielekroniki (GePG) kwa kutumia CONTROL NUMBER ambapo mtawezesha Wananchi kulipia Ankara zao za Maji kwa muda mfupi na kuongeza ufanisi wa Makusanyo ya maduhuli ya Mauzo ya Maji”,ameeleza Ndalichako.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo.
Amebainisha kwamba, Takwimu zinaonyesha kuwa hadi Juni, 2019 kabla ya kuanzishwa RUWASA upatikanaji wa huduma ya maji katika Mkoa ulikuwa asilimia 54.8 kwa maeneo ya Vijijini lakini hadi kufikia Novemba, 2023 baada ya kuanzishwa kwa RUWASA huduma ya maji Vijijini imeimarika sana na imefikia asilimia 66.5.
“Bado kazi ni kubwa ya kuhakikisha maeneo yote ya Vijijini yanafikiwa na huduma ya maji safi na salama. Mkisimamia vizuri miradi iliyopo kutakuwa na uhakika wa uendelevu wa miradi na itaimarisha jitihada za Serikali za kumtua mama ndoo kichwani”,ameongeza.
Katika hatua nyingine Ndalichako amewataka wasimamizi wa CBWSOs kufuata maadili ya utumishi wa umma wanapotoa huduma katika maeneo yao kwa kuepuka kufanya ubadhilifu wa fedha za Umma, kupokea na kutumia fedha za Umma nje ya Mfumo huo, kumuongezea mteja matumizi yasiyo yake na hata kulewa nyakati za kazi, utoro kazini matumizi mabaya ya rasilimali za umma na mienendo isiyo ya kuridhisha katika maeneo yao.
Aidha ameagiza kila chombo kiakikishe taarifa za wateja wote zinaingia kwenye mfumo kwa usahihi, kinyume na hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watumishi wa umma wasio waadilifu.
“Katika maeneo yenu mnasimamia pia makusanyo ya maduhuli, naomba mtambue kuwa hizo ni fedha za umma, ikitokea umezitumia vibaya bila kufuata taratibu za matumizi ya fedha za umma utawajibishwa, na naomba niwaambie kuwa katika hili serikali ya Mkoa iko makini sana, tukikubaini unatumia vibaya fedha za umma hatutakuacha salama, kwani chombo chenu kipo kisheria, Kwa mujibu wa sheria ya maji namba 5 ya mwaka 2019”,ameongeza Ndalichako.
Kwa upande wake, Mratibu wa Fedha kwa Vyombo Vya Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) Tanzania, Adam Mzengi amesema Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki ambao tayari unatumika katika Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Rukwa na sasa Shinyanga utasaidia kuinua sekta ya maji vijijini ambapo hakuna mteja anayetumia huduma ya maji atalipa fedha kupitia mkononi.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi , Julieth Payovela amesema mfumo wa awali ulikuwa unapoteza mapato kutokana na kwamba pesa zilikuwa zinalipwa mkononi na sasa zitalipwa kupitia Namba ya Malipo (Control Number) hivyo hakuna pesa itaenda nje ya mfumo.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema mfumo huo mpya wa malipo kwa njia ya kielektroniki mbali na kusaidia kupata mapato pia utachangia kwa kiasi kikubwa watumiaji wa huduma za maji kulipia huduma kwa wakati kupitia Control Number ambayo inakuwa na muda maalumu wa kulipia huduma.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa CBWSOs Mkoa wa Shinyanga kuhusu kuhamisha Taarifa za CBWSOs kwenda kwenye Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki (GePG) kupitia Mfumo wa Maji’s Billing System and Government Collection Platform).
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wasimamizi wa CBWSOs Mkoa wa Shinyanga kuhusu kuhamisha Taarifa za CBWSOs kwenda kwenye Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki (GePG) kupitia Mfumo wa Maji’s Billing System and Government Collection Platform).
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi wa CBWSOs Mkoa wa Shinyanga kuhusu kuhamisha Taarifa za CBWSOs kwenda kwenye Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki (GePG) kupitia Mfumo wa Maji’s Billing System and Government Collection Platform).
Mratibu wa Fedha kwa Vyombo Vya Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) Tanzania, Adam Mzengi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi wa CBWSOs Mkoa wa Shinyanga kuhusu kuhamisha Taarifa za CBWSOs kwenda kwenye Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki (GePG) kupitia Mfumo wa Maji’s Billing System and Government Collection Platform).
Mratibu wa Uingizaji Vyombo vya Watumiaji Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) RUWASA Makao Makuu Dodoma, George Busunzu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi wa CBWSO Mkoa wa Shinyanga kuhusu kuhamisha Taarifa za CBWSO kwenda kwenye Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki (GePG) kupitia Mfumo wa Maji’s Billing System and Government Collection Platform).
Wasimamizi wa CBWSO Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo kuhusu kuhamisha Taarifa za CBWSO kwenda kwenye Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki (GePG) kupitia Mfumo wa Maji’s Billing System and Government Collection Platform).
Mratibu na Msimamizi wa Mfumo wa Maji kutoka Wizara ya Maji, Masoud Almasi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi wa CBWSO Mkoa wa Shinyanga kuhusu kuhamisha Taarifa za CBWSO kwenda kwenye Mfumo wa Malipo kwa Njia ya Kielekroniki (GePG) kupitia Mfumo wa Maji’s Billing System and Government Collection Platform).