Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) inatarajia
kujenga jengo la ghorofa tano katika Kampasi ya Singida ambalo licha ya kuupendezesha mji wa Singida
lakini pia litaweka huduma za taaluma sehemu moja na hivyo kupunguza wingi wa
majengo.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa taasisi hiyo,
Profesa William Pallangyo amesema hayo kwenye mahafali ya 12 katika kamapsi ya
Singida yaliyofanyika Novemba 17, 2023 mjini hapa.
Amesema ujenzi huo unatokana na mradi wa magezi
ya kiuchumi wa vyuo vya elimu ya juu ambao ni matokeo ya mkopo wa masharti
nafuu unaotekelezwa kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamo jana na
Wizara ya Fedha ambapo Singida kupia TIA Kampasi ya Singida ni miongoni mwa
mikoa nchini iliyonufaika na mpango huo kwa kupata Sh.Bilioni 18.
Profesa
Pallangyo amesema, jengo hilo litakuwa na ghorofa tano likiwa na kumbi
za mihadhara,madarasa kumbi za mikutano pamoja na ofisi linatarajia kuanza
kujengwa Februari mwaka 2024.
” Hadi kukamilika kwa ujenzi huo zitatumika
Sh. Bilioni 16 na kwa sasa kinachofanyika ni uandaaji wa
tathimini ya mazingira,” aliseama Prof. Pallangyo.
Ujenzi huo umekuja hasa kwa kipindi hiki ambapo
Kampasi ya Singida imepiga hatua katika uendeshaji wa mafunzo, huduma za
ushauri wa kitaalam, rasimali watu pamoja na miundo mbinu ya kufundishia na
kujifunzia.
Profesa Pallangyo amesema idadi ya wanaojiunga
kwa mwaka imekuwa ikiongezeka huku akigusia kuwa kwa mwaka wa masomo 2023/2024
TIA Singida imepokea wanafunzi 1443 lengo likiwa ni kufikia 2600 ikilinganishwa
na wanafunzi 1556 kwa mwaka wa masomo ya 2022/23.
Amesema ongezeko la wanafunzi kwa kiasi kikubwa
limetokana na ubora wa elimu unaotolewa na taasisi hiyo na kuwajengea umahiri
unaowawezesha kupata ajira sambamba na kujiajiri.
Amesema Sababu ya pili ni utaratibu wa serikali
kuwapangia vyuo wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu na kukidhi vigezo huku
akifafanua kuwa kwa mwaka wa masomo 2023/24 jumla ya wanafunzi 1170 kutokana
maeneo mbalimbali ya nchi wamejiunga na fani mbalimbali katika chuo hicho.
Ametaja sababu ya tatu kuwa pamoja na ongezeko la
mikopo kwa wanafunzi wa ngazi ya Shahada na kwa mwaka huu pekee jumla ya
wanafunzi 810 watanufaika na mikokopo katika kampasi ya Singida hilo likiwa ni
ongezeko la asilimia 15.9 ikilinganishwa na wachuo 699 waliopata mikopo kwa
mwaka 2022/23.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iramba, Mh.
Suleimani Mwenda ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mh. Peter
Serukamba katika mahafali hayo amesema mafunzo wanayoyatoa kuhusu uhasibu
ununuzi na ugavi, usimamizi wa biashara na uongozi wa rasimali watu unaendana
na mtazamo wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hasani wa kutengeneza Diplomasia ya Uchumi.
Amesema mafunzo wanayoendelea kuyatoa yameendelea
kuboresha ubora wa elimu na kuhamasisha matumizi ya teknolojia hususani Tehama.
Hata hivyo amesema licha ya kufundishwa kuhusu
Tehama lakini matumizi yake bado ni ya kiwango cha chini hasa katika masula ya
kuongeza maarifa kwa mtu mmoja mmoja hasa kwa kundi la vijana.
Ameshauri kuongeza juhudi katika kuwaelekeza
vijana kuhusu matumizi sahihi ya Tehama na kuwa kwa Afrika Mashariki Tanzania
inaongoza katika matumizi ya Tehama lakini watumiaji wakubwa ambao ni vijana chini ya miaka 35
wanaitumia kwa mambo yasiyokuwa na tija.
Akizungumzia kuhusu ajira amewataka wahitimu
kujiongezea thamani kwa kuwa wabunifu kwenye kazi ili wawe na mawanda mapana ya
kupata ajira zisizo kuwa na shaka..
kitaalamu yaani(Career
Development Program), TIA, Imani Matonya akiwajibika.
Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakirusha kofia juu kuonesha furaha
zao katika mahafali ya 21 ya taasisi hiyo.
Picha za matukio mbalimbali ya mahafali hayo zikichukuliwa. |
ya Ushauri wa wizara na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA) Profesa. William Pallangyo.