MWANDISHI WETU, LINDI
WAZIRI
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemuhakikishia Mnufaika wa Fidia inayotolewa na
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Halima Sheikh Mbwana, kuwa ataendelea
kuishi kwa furaha ikiwa ni pamoja na kutunza familia yake kwani WCF ipo.
Mhe.
Majaliwa ameyasema hayo kwenye Mkutano wa 7 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF), mjini Lindi, Novemba 13, 2023, baada ya kusikiliza ushuhuda wa mnufaika
huyo aliyepata ulemavu wa kudumu kufuatia kukatika mkono baada ya basi la
abiria alilokuwa akiliendesha, kupinduka Mei 22, 2022, wakati likiwa safarini
kutoka Songea kuelekea Dar es Salaam.
“Mwenyezimungu
ana matakwa yake na kila mmoja amempangia jambo lake na inshaallah, utaishi,
utatunza familia yako kwani WCF wapo.” Alimuhakikishia Bi. Halima
Waziri
Mkuu pia aliipongeza WCF kwa kumfuata Bi. Halima hospitalini baada ya kuarifiwa
kuwa amepata ajali na kuumia.
“Nawashukuru
WCF kwa kutekeleza wajibu wenu, wa kumfuata mgonjwa hospitalini na
kujitambulisha kwamba sisi ni ule Mfuko wa Fidia kwa Watumishi wanaoumia katika
kazi na kutambua kwamba dada yetu alikuwa kazini.”
Aidha
Waziri Mkuu aliwahimiza waajiri kujisajili na Mfuko kwa manufaa yao na
wafanyakazi wao, kwani ushuhuda uliotolewa na Bi, Halima mwenye familia ni
ujumbe tosha kwa wao kufanya hivyo.
“Na
ametoa ujumbe hapa kwa waajiri wote, jiungeni na WCF kwa usalama wa Wafanyakazi
wenu wanapoumia wakiwa kazini watalipwa fidia. Leo dada yetu anapata mafao yake
kila mwezi na yanamsaidia kuendesha maisha yake.” Alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Awali
wakati akitoa ushuhuda, Bi. Halima aliishukuru Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo
ambao umeweza kumfariji baada ya kukumbwa na changamoto hiyo.
“Nilipopata
ajali na kupelekwa hospitali, watu wa WCF walinitembelea na kunieleza jinsi
Mfuko utakavyonihudumia, na kweli wamenihudumia kwa matibabu hadi kupona na
kunipatia kiungo cha bandia” aliongeza.
Halima
amesema licha ya huduma hizo, bado WCF inamlipa mafao kila mwezi
yanayomuwezesha kuendesha maisha yake na familia yake.
“Sikuwahi
kuwaza kama nitakuja kuwa na faraja, nilikuwa na asilimia 90 ya furaha na WCF
wamejazia asilimia 10 kwa kuniweka vizuri na kunionyesha upendo, hivi sasa
ninatembea, ninadunda kwa furaha.” Alisema.
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza kwenye mkutano wa 7 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Mkoani Lindi Novemba 13, 2023