Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa Habari Jijijini Dodoma
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius .K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kilichopo wilaya ya Butiama Mkoani Mara Prof. Lesakit Mellau akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake Butiama.
………….
Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius .K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kilichopo wilaya ya Butiama Mkoani Mara kimejipanga kuhakikisha jamii inayokizunguka chuo hicho inanufaika katika kilimo cha kisasa ili tija ya shughuli hizo iongezeke.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lesakit Mellau, ambapo amesema mkakati huo unalenga kuwakwamua kiuchumi wakulima wanaoishi jirani na chuo ambao bado wanatumia njia za jadi kuendesha shughuli za kilimo pasi na kupata matunda ya jitihada zao.
“Kwa mwaka huu wa masomo chuo kimejipanga kuhudumia wanafunzi wapatao mia nne huku endapo kitapokamilisha ujenzi wa miundombinu kwa asilimia mia moja basi kitakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi elfu nne mia tano hivyo itasaidia kufungua nafasi ya ajira kwa wenyeji wa Butiama”. alisema Prof.Mellau
Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Butiama Mhe.Jumanne Sagini amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kujengwa kwa Chuo kikuu cha Mwalimu Juliasi Nyerere cha kilimo na Teknolojia.
Ndoto za Chuo hicho zilianzishwa na Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julias Nyerere na Kuja kufanikishwa na Raisi wa awamu ya Sita.
“Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya sita kwa kutimiza ndoto za mda mrefu za mwalimu nyerere na wanabutiama kwa ujumla kwani uwepo wa chuo hiki unaenda kufungua Fulsa nyingi za wanabutiama” alisema Naibu Waziri Sagini
Kwa upande wao wakazi wa Butiama wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwaletea chuo hicho kwani watoto wao watapata Ujuzi kwa umbali mdogo na wataweza kujikwamua kiuchumi kutokana na uwepo wa wanachuo.
“mimi naishukuru serikali ya mama Samia kwa kutuletea chuo hiki ili watoto wetu wapate ujuzi kwa umbali mdogo hvyo tuanamuomba mama samia azidi kutuletea Miradi mingine ili tujikwamue na umaskini. Alisema Mangole Marwa